leo katika somo letu la urembo ningependa kuangalia katika utunzaji wa nywele bila ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kemikali ambayo yamesababisha kwa kiwango kikubwa matatizo katika ukuaji wa nywele kama nywele kukatika,kunyonyoka,kupooza katika ukuaji n.k
Hina ni moja kati ya mimea ambayo watu wengi hasa wanawake huitumia katika kujiremba hasa kujichora maongoni bila kutambua kuwa mmea huo huweza kusaidia katika utunzaji wa mwelw zao kwa kiasi kikubwa.
Embu tuanze maandalizi ya Hina.
MAHITAJI:-
- Hena vijiko vitatu vya chakula.
- Kipande cha ndimu ama limao.
- Maji ya chai kiasi kidogo.
- Glavu mbili mpya.
NAMNA YA KUFANYA:-
- Vaa clavu ili mikono yako isiharibiwe na hina.
- Changanya hina na viongo vyake hakikisha haiwi nyepesi sana wala nzito sana.
- Gawa nywele zako katika mafungu manne,kisha paka ina yako kwa uangalifu ili isichafue uso wako.
- Hakikisha unakaa nayo kwa muda usiopungua lisaa limoja.
- Zikiwa tayari,hakikisha unaosha vizuri na kukausha nywele zako kwa taulo lililo safi.
Ningependa kukushauri utumia mafuta yasiyo na kemikali yatokanayo na vitu asili kama mimia,matunda nk.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO