Habari Zetu

Showing posts with label simulizi zetu. Show all posts
Showing posts with label simulizi zetu. Show all posts

WACHAGA MPOOOO?



Mnyakyusa mmoja aliwaalika watu
katika mazishi ya mama yake. Baada ya kushusha jeneza wakatia ndani ya kaburi viazi, mchele na kuku kadhaa.
Mhaya mmoja akauliza, 'Vya nini hivyo?'
Akaambiwa, 'Wafu huenda safari ndefu sana, hivi atakula njiani'.
Mhaya akazama kwenye wallet, akatoa laki 2, akaidondoshea akisema, 'vikiisha hivyo atanunua vingine'.Mkurya mmoja akadondoshea laki moja
akasema, 'Isipotosha ataongezea hii'
Mchaga akatoa cheque book, akaandika cheki ya laki 5, akachukua ile laki 3 kwenye kaburi na kuacha cheki akisema,'bora ukachukue hela mbele ya safari kwa
cheki. Vibaka wasije WAKAKUUA bure'.
Shikamoo wachaga!

Hii muhimu: Kutokana na ukosefu wa ajira wanachuo kikuu walazimishwa kurekodi picha za Ngono.

Sunday Bekunda

Hivi karibu kundi hilo linalosafirisha watu lilipita katika vyuo vikuu kadhaa nchini Uganda na kuwaahidi wanafunzi kuwa lingewatafutia kazi Ulaya na Marekani, kwani lina uzoefu wa kutosha na kazi hiyo. Mmoja wa vijana ‘waliobahatika’ kupata nafasi ya kwenda Ulaya kufanya kazi ni Sunday Bekunda (25), mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.
Kwa bahati mbaya ‘neema’ ya kwenda Ulaya iligeuka balaa baada ya kutekwa na kulazimishwa kufanya ngono na wanawake mbalimbali huku akirekodiwa kwenye kamera za video.
“Ilikuwa ni Januari 2013, nilipokutana na mwanaume mmoja anayeitwa Charles kutoka katikati ya Jiji la Kampala, ambaye aliniahidi kunipeleka Kenya kufanya kazi katika kiwanda.
“Sikujua kuwa Charles alikuwa msafirisha watu. Alikuwa anaonekana kama mzazi wa makamo aliyefanya kazi kwa miaka mingi.
“Nilifungua moyo wangu na kumweleza changamoto nyingi ninazopitia na namna nilivyo hangaika kutafuta kazi ili nipate fedha za kulipia masomo ya ziada. Kwa kifupi ni kama nilikuwa namwambia Charles kuwa sikuwa natafuta kazi bali nilikuwa nataka kazi yoyote.”
Safari ya Kenya
“Siku iliyofuata nilikuwa tayari kwa safari na nilimkuta Charles akiwa kwenye gari la binafsi aina ya Toyota Noah. Alikuwa pamoja na wasichana sita na wavulana wawili. Alituambia kuwa tutaingia Kenya kwa kupitia mpaka usio rasmi unaoitwa Chepskunya.
“Tukiwa njiani, Charles alikuwa anaongea sana na kutusisitizia kuwa ‘tusimwangushe’ tukifika huko. “Tulipofika Kenya walituchukua na kutuingiza kwenye nyumba moja nzuri ya makazi ya watu, hapo tulikutana na wenzetu 15, wavulana wawili kutoka Rwanda na Wakenya 13.”
Kutekwa
“Charles alituacha hapo tukiwa chini ya mwanamke mmoja na wanaume wanne wenye miili iliyojengeka vyema. Watu hao walianza kutupiga makofi na kutulazimisha tuvue nguo. Ndipo nilipobaini kuwa kilichoonekana kama ni safari sasa imegeuka utekaji.
“Baada ya kupigwa tuliambiwa tutoe mifukoni kila kitu tulichokuwa nacho na kuweka juu ya meza. Nilishtushwa nilipoona vyeti vya wanafunzi wa Uganda kutoka Vyuo Vikuu vya Kyambogo, KIU (Kampala International University), Nkumba na UCU (Uganda Christian University). Hata vyuo vya Kenya vilikuwapo.
“Mwanamke alitutishia kutuua kama tusingetii walichosema. Kudhihirisha alichokuwa anamaanisha, alituonyesha mkanda wa video wa mtu akiuawa na kupasuliwa tumbo.
“Halafu wakaweka video vyingine iliyotuonyesha biashara tutakayokuwa tunaifanya, ambayo ni kuigiza picha za ngono.”
Ratiba ya kufanya ngono
“Walituongoza hadi ghorofa ya juu na kutuweka katika vyumba tofauti. Katika chumba nilichokuwepo aliingia mtu na kuniambia nitoe nguo kisha akanipa chupi tatu zinazobana.
“Hicho chumba kilikuwa na mwanga mkali na kamera za CCTV katika kila kona. Baadaye wakamleta Bridget, mmoja wa wasichana niliotoka nao Uganda, kisha wakaniambia kuwa nipo huru kufanya naye ngono. Walipoondoka na kufunga mlango, Bridget alianza kulia na kupiga kelele.
“Matukio mabaya yalianza rasmi siku iliyofuata wakati yule mwanamke alipoingia kwenye chumba changu akiwa ameshika mikanda mitatu ya ngono. Baadaye waliletwa wanawake na wanaume niliokuja nao nikaambiwa nifanye nao ngono wakati watu wengine wakirekodi kwa kutumia kamera kubwa.
“Nilipoishiwa nguvu, yule mwanamke alitoka nje na kurudi halafu alinichoma sindano yenye dawa ambayo ilinifanya nipate nguvu tena na kuendelea. Nikapewa ratiba ya kulala na wanawake asubuhi, wavulana jioni (mashoga) na wanawake watu wenye umri mkubwa usiku.
“Wanawake hao walikuwa wanawalipa wale jamaa ili tufanye nao ngono. Kuna wakati nilikuwa nalazimishwa kulala na wanawake saba kwa siku huku nikipata maumivu makali.”
Mauaji
“Baada ya wiki tatu wote tuliitwa sebuleni na kupewa taarifa kuwa mmoja wetu, aliyeitwa Sam Muteesi kutoka Uganda, alikuwa amekataa kuwatii kwa hiyo alitakiwa auawe mbele yetu. Walimfunga kwenye kiti, japokuwa alikuwa akiomba sana msamaha walimfunika  usoni kwa kutumia begi hadi alipokufa.
“Kwa kipindi chote cha Januari na Februari 2013, nilikuwa nikifanya ngono za kila aina kila siku huku nikitumia dawa za kulevya na pombe.
“Mwanzoni mwa Machi, Charles alikuja kwenye chumba changu na kuniambia kuwa ninatakiwa kwenda kuoa Uingereza. Halafu akafungua kompyuta yake na kunionyesha picha ya mwanaume mzee mzungu.
“Akaniambia nipite mbele ya kompyuta hiyo nikiwa nimevaa chupi nilizopewa ili huyo mzungu anione (kupitia Skype) kama nifaa.
“Huyo mzungu alinipenda, hivyo Charles akawa amepata ‘dili’ ambayo ingenipeleka Uingereza, lakini kwa kuwa sikuwa Mkenya nilitakiwa nirudi Uganda kuchukua hati ya kusafiria.
Atoroka
“Wakati tukivuka mpaka kuingia
Uganda, nilifanikiwa kukimbia pale Mbale tulipokuwa tumesimama kunywa chai. Nilitoa taarifa yangu na kufunguliwa faili namba SD REF 65/19/03/2013. Kwa kuwa Charles alikuwa mtu mwenye nguvu (kifedha) hakufanywa chochote.
“Kutokana na mateso niliyopitia nilikuwa kama kichaa, nililazwa katika Hospitali ya Vichaa ya Butabika na nilipewa matibabu kati ya Agosti na Desemba 2013.
“Pia nilipimwa vipimo vingine na kugundulika kuwa nilikuwa na maambukizi yote makubwa ya magonjwa ya zinaa.“Nimeamua kusimulia habari yangu kama sehemu ya kampeni ya kuwaonya vijana wa vyuo vikuu kuwa makini na watu wanaowaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi.”

Njia rahisi ya kupata utajiri kwa wavuta sigara.




Girl: unavuta sigara?
Boy: navuta

Girl: umevuta kwa miaka mingapi sasa?
Boy: miaka 10

Girl: kwa siku unavuta pakti ngapi?
Boy: 3

Girl: pakti moja shilingi ngapi?
Boy: sh 600

Girl: kwahiyo siku 1 pakti 3 unatumia sh1800
Boy : ndiyo

Girl: sh 1800 mara siku 30(mwezi moja)
Boy: ni sh 54,000 kwa mwezi

Girl: hiyo sh 54,000 mara miezi 12(mwaka1)
Boy: ni sh 648000(laki 6 na elfu 48 kwa mwaka)

Girl: zidisha mara miaka 10.
Boy: million sita na kuendelea

Girl: huoni usingevuta sigara ungeshanunua gari?
Boy: we unavuta sigara?

Girl: hapana
Boy: pumbavu kweli.! Gar lako liko wapi?

beib wa word cup hoi.






World cup hii
Demu; Baby kwanini hawa blue(Bosnia) wamefunga 2 na hawa akina Messi(Argentina) wamefunga 1 lkn inaonyesha akina Messi wameshinda mechi?
Jamaa; hawa blue goli 1 wamejifunga
Demu; kwahiyo lzm wafunge goli la huku?
Jamaa; ndiyo
Demu; sasa mbona Messi nae kafunga goli la huku?
Jamaa; halftime huwa wanabadilishana magoli
Demu; aanhaaa kumbe!!!
Demu; halaf baby si ulinambia uwanjani wachezaj mwisho 11?. sasa mbona yule kavaa no 15?
Jamaa; jezi unavaa no yoyote
Demu; sasa baby km golikipa anaruhusiwa kushika mpira na mkono kwanini asikimbie nao mpk mbele kisha akampa Messi akafunga lkn mpk apige huku huku?
Jamaa; mpenzi hebu tulale mpira umeshaisha kesho kazini

Hatari ya mapenzi ya Facebook




Dada mmoja alikutana na kijana mmoja kwa njia ya facebook na wakapendana hapa mtandaoni.
Baada ya kuchati kwa muda mrefu wakaamua waende kuonana na hatimaye wakaona na binti kukaribishwa katika chumba alichopanga kijana huyo.
Alipofika akaanza kuhisi kuwa amefanya maamuzi yasiyo sahihi kwenda pale kwani chumba kilinuka harufu ya pombe na bangi na pia kulikuwa na vijana wengine wapatao wanne wakiwa wamelewa pale.
wakamwingilia kinguvu dada yule na kisha baada ya kugundua kapoteza fahamu wakamtupa nje karibu na barabara na dada alipopata fahamu kwa aibu akaondoka na hakumwambia mtu na kukaa kimya.
Miezi michache baadae akagundua kuwa ni mjamzito na kwa sheria za ile nchi akatakiwa kufukuzwa katika ile jamii kwani amefanya kosa la kuiabisha jamii kupata ujauzito bila muda wake muafaka kufikia.
Siku chache baadae ikaja onekana maiti yake ikiwa pembeni ya mji ule katika nyumba moja akiwa na karatasi mkononi iliyoandikwa:
" Kwa wadogo zangu miliobaki, mitandao ya kijamii ina faida kubwa na hasa zake pia... kamwe msiwe wepesi wa kufanya maamuzi na kuja kuwa wahanga wa matatizo niliyokumbana nayo mimi dada yenu.... Nawapenda sana"
Sala kwa ajili yako
Mitandao ya kijamii itakupa marafiki watao kupanua mawazo ya kuziboresha kazi zako na sio watakao kuharibia kazi zako na maisha yako pia.
Kila rafiki atakuwa hazina ya mafanikio yako nawe utapata busara na hekima ya kuwatambua marafiki feki na wale wenye nia njema

Mwalimu na ndoto za wanafunzi

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza
wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo
niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo....
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanaopenda kusafiri kwa anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe Jason??
JASON: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa
sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……” Akameza mate kisha akaendelea…. “Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea
ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa
natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa Jason.!

Story ya Mkinga,Mchaga na Mchina Hotelini

Wafanya biashara wa3 Mkinga, Mchaga na Mchina.
Wakiwa kwenye mgahawa fulani town. Wakati wanakula nzi akatua kwa mkinga, mkinga akamfukuza, akaenda kutua kwa mchaga nae akamfukuza.
Akaenda kutua kwa mchina kwenye pua yule mchina akamtime baada ya muda akamkamata na kumuweka mdomoni na kumtafuna,
Mkinga na mchaga waliona wakachuna tu. Mara ya pili akaja mwingine akatua kwa mkinga, akamfukuza tena. Akatua kwa mchaga, akamuangaliia yule nzi akamdaka na kumgeukia mchina na kwumwambia, "shilling ngapi aisee nikuuzie?"

Hasara ya Mbunge Mchelewaji Kanisani

Bahati mbaya, mbunge
alichelewa kufika .... Mc
akamwomba padri aseme
machache wakati wanamsubiri mheshimiwa mbunge....
Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi,
aliongea:.
"Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika kanisa hili kwa mara
yakwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza kuungamisha.
Mtu wa kwanza kabisa
kumuungamisha alinishangaza sana."
Akameza mate kisha akaendelea,
"Mtu huyo alipokuja kuungama alisema amemwibia bosi wakeTV, amemwibia ndugu yake
pesa za urithi, akiwa shuleni
aliwahi kukojoa kitandani
akamsingizia mwenzie, amezini na mke wa jirani yake, na pia alimlazimisha house girl wake kufanya nae mapenzi.
Nikapata picha kuwa kumbe watu wa
kanisa hili ndivyo walivyo,
nikasikitika sana.....
Lakini baadae nikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawatendi dhambi mara kwa mara.
Yule muumini wa kwanza
aliyekuja kutubu alitaka
kunifanya niwafikirie vibaya
kumbe nyie ni watu wema. Yule alikua na dhambi zake
mwenyewe..."
Wakati Padri akiongea hayo
mara Mheshimiwa Mbunge
akawasili, Padri akakatisha
maongezi na mbunge akaanza kuhutubia.
Akaanza kwa kusema:-
"Ndugu wapendwa, naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kwani nilikuwa na majukumu makubwa
ya kiserikali....
Kisha akaendelea...
"Pia ninayo furaha kubwa kwa kunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu.
Mimi nina bahati sana kwani Padri huyu alipokuja hapa, mimi ndiye nilikuwa muumini wa kwanza kabisa kwenda kutubu kwake..."
Kanisa zima vicheko...!!
Tunajifunza nini!?:
Tujifunze kuwahi kwenye matukio kwani huwezi kujua umuhimu wa
lililokupita.!...
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency