Home » » 'Singlet' kivazi kinachohitaji usafi zaidi

'Singlet' kivazi kinachohitaji usafi zaidi

 


                     KUNA wanaume nawasifu kwa kuzingatia usafi wa mavazi yao na hata muonekano wao licha ya kuwa wengine wameamua kuliweka kando kidogo suala hili.
Unapokuwa mtanashati unakuwa na kila sababu ya kujiamini.
Usafi wa mwili umekuwa ukisisitizwa sana kutokana na ukweli kuwa usafi ni afya na muhimu kwa kila moja kuwa na tabia ya kuwa msafi wakati wote.
                     Usafi ni pamoja na kuoga na kutakata vizuri, kutorudia kuvaa nguo ambayo imevaliwa na inanuka jasho na hata kunyoosha nguo vizuri kabla ya kuvaliwa.
Singlet pamoja na kuvaliwa ndani ya shati pia zimekuwa zikivaliwa zaidi na wanamichezo ikiwemo mieleka na wale wa mbio ndefu.
Wengi wanavaa singlet ndani ya nguo nyingie iwe kwa wanaume au kwa wanawake
                     "Unaponunua singlet unazingatia zaidi ubora na kitambaa kilichotumika kutengeneza nguo hizo kama ni pamba au aina nyingine ya kitambaa, lakini wanaume wengi wanapendelea pamba zaidi" anasema mkazi mmoja wa Jijini Dar es salaam.
                        Uvaaji wa singlet unatakiwa kuzingatia zaidi usafi kutokana na ukweli kuwa nguo hiyo imekuwa ikivaliwa sana na wakati mwingine huathiriwa zaidi na jasho linalotoka mwilini.
Pia ni vizuri kuhakikisha usafi wa kwapa ili kuweza kuhakikisha kuwa,singlet yako inakuwa katika hali ya usafi muda wote na ili isiwe tabu kwako kuinua mkono kwani wengi wanaficha kwapa zao kutokana na uchafu kitu ambacho si kizuri.
                         Uvaaji huo unazingatia sana rangi kutokana na matakwa ya mvaaji ila wengi wanapendelea rangi nyeupe.
Nguo yoyote ya rangi nyeupe ni nzuri na inapendeza ikivaliwa kwani rangi nyeupe pia huonyesha kipimo cha usafi wako.
                          Kwa kina dada wanaopenda kuvaa singlet nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa kwapa zao zinakuwa safi ili kuweza kuwa huru zaidi.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency