Home » » Hasara ya Mbunge Mchelewaji Kanisani

Hasara ya Mbunge Mchelewaji Kanisani

Bahati mbaya, mbunge
alichelewa kufika .... Mc
akamwomba padri aseme
machache wakati wanamsubiri mheshimiwa mbunge....
Padri hakujipanga kusema kitu lakini kwa kujitahidi,
aliongea:.
"Wapendwa, naikumbuka sana siku nilipofika katika kanisa hili kwa mara
yakwanza, ila nilipata mshangao siku nilipoanza kuungamisha.
Mtu wa kwanza kabisa
kumuungamisha alinishangaza sana."
Akameza mate kisha akaendelea,
"Mtu huyo alipokuja kuungama alisema amemwibia bosi wakeTV, amemwibia ndugu yake
pesa za urithi, akiwa shuleni
aliwahi kukojoa kitandani
akamsingizia mwenzie, amezini na mke wa jirani yake, na pia alimlazimisha house girl wake kufanya nae mapenzi.
Nikapata picha kuwa kumbe watu wa
kanisa hili ndivyo walivyo,
nikasikitika sana.....
Lakini baadae nikakuta kumbe watu wa hapa ni wazuri sana na hawatendi dhambi mara kwa mara.
Yule muumini wa kwanza
aliyekuja kutubu alitaka
kunifanya niwafikirie vibaya
kumbe nyie ni watu wema. Yule alikua na dhambi zake
mwenyewe..."
Wakati Padri akiongea hayo
mara Mheshimiwa Mbunge
akawasili, Padri akakatisha
maongezi na mbunge akaanza kuhutubia.
Akaanza kwa kusema:-
"Ndugu wapendwa, naomba mniwie radhi kwa kuchelewa kwani nilikuwa na majukumu makubwa
ya kiserikali....
Kisha akaendelea...
"Pia ninayo furaha kubwa kwa kunipa nafasi hii kuhutubia kwa niaba yenu.
Mimi nina bahati sana kwani Padri huyu alipokuja hapa, mimi ndiye nilikuwa muumini wa kwanza kabisa kwenda kutubu kwake..."
Kanisa zima vicheko...!!
Tunajifunza nini!?:
Tujifunze kuwahi kwenye matukio kwani huwezi kujua umuhimu wa
lililokupita.!...
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency