Ugonjwa katika njia ya mkojo (U.T.I) ni ugonjwa unaoshambulia njia za mkojo na husipotibiwa au kuchukuliwa tahadhari mapeme huweza pia kushambulia kibofu na figo hatimaye kuleta madhara zaidi.
Ugonjwa huu hutimbiwa kwa kutumia mchanganyiko wa dawa tofauti ambazo hutolewa kwa ushauri wa daktari.
Ili kuepuka ghalama na usumbufu unaosababishwa na ugonjwa huu unaweza kuzingatia mambo yafuatayo ili huweze kujikinga na kuzuia ugonjwa huu.
- Kunywa maji mengi kiasi cha glasi 6 mpaka 8 itakusaidia kukojoa mara kwa mara na hupunguza idadi ya maambukizi katika njia ya mkojo.
- Epuka vyakula na vinywaji vinavyoweza kukuweka katika hatari ya maambukizi, kama kahawa na pombe ambavyo hupunguza kinga za mwili.
- Safisha njia ya mkojo(Urethra) kila baada ya kukojoa na kufanya tendo la ndoa kuanzia mbele kuelekea nyuma ili kuepuka wadudu katika njia ya haja kubwa kuingia katika njia ya mkojo
- Epuka dawa na poda zinazopuliziwa katika njia ya haja ndogo au kuingiza vitu au vidole pasipostahili huweza kuchubua sehemu hizo na kufanya urahisi wa maambukizi.
- Vaa nguo za ndani asili ya pamba na zisizobana sana kuacha hewa ya kutosha ili kupunguza maambukizi.
- Usibane mkojo kila unapojisikia kwenda haja fanya hivyo ili kuepuka wadudu kusukumwa na kusambaa katika kibovu na figo.
- Usilale au kukaa kwa kukunja miguu muda mrefu kwani utawatengenezea mazingira mazuri wadudu ya kuzaliana na kusambaa sehemu za juu za mwili,
- Kondom za kike pamoja na chemikali za kuzuia mimba hupunguza kinga na huwezo wa mwili hivyo kusababisha wadudu kuongezeka.
Dalili zikizidi muone daktari kwa ushauri na dawa ili kumaliza tatizo.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO