Home » » Mwanamuziki wa Injili Happy haukumiwa kifungo cha miezi mitatu.

Mwanamuziki wa Injili Happy haukumiwa kifungo cha miezi mitatu.







Habari za Uhakika zilizopo mjini Mbeya zinasema kuwa Mwanamuziki wa Injili nchini Tanzania anayejulikana kwa jina la Happy Kamili anayetamba sana na wimbo wake "Mpango Wa Mungu" na "Jina Kubwa" amehukumiwa kifungo cha Miezi Mitatu Jela bila faini katika Mahakama Ya Mwanzo Mkoani humo kwa Kosa la Kusababisha ajali ya barabarani.






Kesi hiyo iliyokuwa imeanza kusikilizwa mwezi January Mwaka huu, siku ya jana imetolewa hukumu kwa Mwanamuziki huyo kupatikana na hatia ya kusababisha ajali kwa kugonga gari lingine kwa nyuma. Mwanamuziki huyo baada ya Kukiri kutenda kosa hilo mahakamani alipatikana na hatia ya Hakimu alitoa Hukumu ya Miezi Mitatu Jela pasipo kutoa Hukumu Mbadala ya Faini.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency