Home » » Picha Muhimu : Watu watano wafa katika ajari ya mafuta mbagara.

Picha Muhimu : Watu watano wafa katika ajari ya mafuta mbagara.










Watu watano wamepoteza maisha na wengine 6 wako katika hali mbaya kati ya majeruhi 17 wa ajali ya moto uliosabishwa na watu waliokuwa wakiiba mafuta baada lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta ya Petroli kuanguka karibu na makazi ya watu eneo  Mbagala charambe jiji Dar es salaam.


Kutokana na moto huo baadhi ya wafanyabiashara waliopoteza mali zao ambapo wengine mpaka sasa hawajajua thamani ya mali zililotekea ambapo mmoja wa wafayabiashara Bwana Ali Mohamed mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi amedai kupoteza malizenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 70, huku wengine wakitaka bima ya lori itumike kufidia mali zilizopotea. 

 






Akielezea tukio lilivyotokea mmoja wa wagonjwa Bwana Rajabu Selemani amesema baadhi ya watu walioungua akiwemo yeye alikuwa anapita barabarani akitokea kazini ndipo alipokuta barabara imetapakaa mafuta ya petroli na baadae moto mkali ghafla ukaanza kuwaka na kuwaunguza miguuni.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency