Home » » Mwenyekiti mwenza wa ukawa aliomba bunge kuahirisha shughuli zake ili kujadili ripoti ya Escrow

Mwenyekiti mwenza wa ukawa aliomba bunge kuahirisha shughuli zake ili kujadili ripoti ya Escrow



Mwenyekiti mwenza wa umoja ya Katiba ya wananchi-UKAWA -Mheshimiwa James Mbatia ameliomba bunge  kuahirisha shughuli zake za kawaida,ili kujadili tukio la wizi na usambazaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayohusu uchunguzi wa wizi wa shilingi bilioni 321 fedha zilizokuwa katika ya akaunti ya tegeta ya Escrow.

Hoja hiyo ya Mheshimiwa Mbatia ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa imefuatia taarifa kuwa ripoti hiyo  imesambaa mitaani   mjini Dodoma  huku  kurasa  zikiwa zimenyofolewa  ili kupoteza ushahidi.

Mheshimiwa Mbatia amesema inavyoonekana taarifa hiyo imeib wa na kusambazwa baada ya kupokelewa na Ofisi ya Katibu wa Bunge kinyume cha kifungu namba 31 kifungu kidogo cha Tisa ( G) cha Sheria,ya haki,kinga na madaraka ya Bunge ambacho kimeainisha ni kosa kwa mtu yeyote kusambaza nyaraka iliyoandaliwa kuwasilishwa bungeni kabla ya wakati wake.

Akijibu  hoja hiyo ,Spika wa Bunge  Mheshimiwa  ANNA MAKINDA amesema ofisi ya ke kwa kushirikiana na Jeshi la P olisi imezuia kumwachia mtuhumiwa wa usambazaji wa taarifa hiyo,ili aweze kusema mahali alipo itoa taarifa  hiyo  pamoja na vifaa alivyotumia ,ili viweze kukamatwa.

Hata hivyo maelezo hayo ya spika hayakukubaliwa na  idadi kubwa ya wabunge wa UKAWA ambao wameomba  mwongozo wa spika  kwa maelezo kuwa  mjadala huo unalenga kujadili haki,kinga na madaraka ya bunge ,baada ya baadhi ya wabunge kupitishiwa nyaraka za kuchafuliwa ,chini ya milango wakwemo wajumbe wa kati ya  PAC.

Waziri kivuli wa  wizara ya nishati na madini ambaye pia ni miongoni mwa viongozi wa UKAWA  Mheshimiwa John Mnyika  ame dai mtuhumiwa huyo ana u husiano  na  mmoja na viongozi  wa  wizara  hiyo, hivyo amemtahadharisha spika kuwa iwapo mtuhumiwa huyo atapelekwa mahakamani ,badala ya kujadiliwa bungeni ofisi  ya spika itaonekana kuhusika.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency