Home » » Katibu UVCCM Meru afariki kwa ajali

Katibu UVCCM Meru afariki kwa ajali

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (Uvccm) Wilaya ya Meru, Lucy Bongele amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa, Onesmo ole Nangole alisema kuwa ajali hiyo ilitokea eneo la Kimba, Ngorongoro na kuwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Katibu wa Uvccm mkoa, Mwajuma Rashid na dereva wao, Omar Mzava.
  Ajali hiyo ilitokea wakati katibu huyo akiwa ameambatana na viongozi wenzake kwenda kumsimika Kamanda wa Uvccm wilaya ya Ngorongoro, Bruno Kawasange katika kijiji cha Makoroma.
  Naye Katibu wa CCM wilaya ya Karatu, Kulwa Milonge alisema kuwa majeruhi hao waliwahishwa hospitali ya Meru baada ya ajali na kupatiwa huduma ya kwanza kabla hawajahamishiwa Arusha kwa matibabu zaidi.
 Milonge alisema: “Hali za majeruhi ni mbaya na Bongole alifariki baada ya kuchomoka kutoka ndani ya gari na kuangukia nje hali iliyosababisha apoteze maisha papo hapo.”
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency