Home » » watuhumiwa wa ugaidi walipopandishwa kizimbani.

watuhumiwa wa ugaidi walipopandishwa kizimbani.


Na Mpenda Mvula,Songea.
WATU saba wanaodaiwa kuunda mtandao wa kigaidi Songea mkoani Ruvuma wameshakamatwa na muda wowote kuanzia sasa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowabili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa wanadaiwa kuhusika na matukio matatu tofauti ya urushwaji na utegaji wa mabomu ya kienyeji.

Alifafanuwa kuwa tukio la kwanza lilitokea Septemba 16 mwaka jana majira ya saa 1.30 jioni huko katika eneo la Misufini kikundi hicho kinachojihusisha na ugaidi kiliwarushia Askari polisi waliokuwa doria bomu la kienyeji la kurushwa ambalo liliwasababishia askari watatu kujeruhiwa.

Alisema kuwa katika tukio lingine ambalo lilitokea Oktoba 27 mwaka jana majira ya saa 10 jioni lilichimbiwa ardhini bomu katika eneo la Mshangano ambalo hutumiwa kama kituo cha ukaguzi wa magari yanayotoka na kuingia Songea mjini na askari wa kikosi cha usalama barabarani kando kando mwa Barabara inayotoka Songea kwenda Njombe kwa lengo la kuwalipua askari wa kikosi hicho.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kuwa pia kabla hawajatimiza hazma hiyo askari wa usalama barabarani waliokuwa kwenye eneo hilo waliligunduwa bomu hilo likiwa limechimbiwa ardhini na jeshi la polisi kwa kushilikiana na jeshi la wananchi (JWTZ) baada ya kupata taarifa hiyo walifika kwenye eneo la tukio na waliweza kuliteguwa bila kuleta madhara.

Alilitaja tukio lingine la tatu kuwa lilitokea Disemba 25 mwaka jana majira ya 1.30 usiku katika eneo la Majengo Kotazi kikundi hicho cha ugaidi pia kilidhamilia kuwarushia bomu askari waliokuwa wanafanya doria ambapo mtu mmoja kutoka katika kikundi hicho alijaribu kuwarushia bomu askari hao na kabla hajarirusha lilimlipukia yeye mwenyewe na kufariki Dunia papo hapo na kusababisha askari polisa wawili kujeruhiwa vibaya.

Alieleza zaidi kuwa timu ya upelelezi toka ndani ya jeshi la Polisi kwakushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimeweza kubaini eneo linalotumika kwa mafunzo ya kigaidi na kikundi hicho na kwamba mpaka sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo na wanatarajia kupanda mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency