Bibi mmoja ambaye jina
lake halikuweza kufahamika amekutwa katika mazingira ya kutatanisha jijini Mwanza yaliyojenga mitazamo tofauti kutokana na imani za watu wengi
Bibi huyo pindi alipokuwa akiojiwa na baadhi ya watu mbalimbali waliomzunguka alidai kuwa ametokea mjini Bariadi na alishushwa na wenzake wanne waliokuwa katika safari zao usiku ndani ya chombo chao cha asili maarufu kama Ungo baada ya kugombana kwa muda mrefu.

\
Bibi huyo alikuwa akionekana eneo maarufu hospitalini sekoutoure akiangaika kwa kuranda huku na kule,aidha mitazamo ya watu tofauti hasa kundi lililodai kuwa bibi huyo ni mwaka na kutaka kujichukulia sheria mkononi ya kutaka kumpiga mawe lilifuta hisia za chombo cha dola ambao walifika muda mchache na kuwatawanya watu wote waliokuwa wamemzunguka.
 |
Bibi akiwa mpweke baada ya kutawanywa watu wote waliomzunguka |
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO