Habari Zetu

Showing posts with label News. Show all posts
Showing posts with label News. Show all posts

WATANZANIA POPOTE MLIPO MPIGIENI KURA KIJANA HUYU,MTANZANIA PEKEE ANAYESHIRIKI SHINDANO LA BIASHRA DUNIANI


 Mtanzania popote  ulipo  hakikisha  unampigia  kura  Deo Polycarp Goodluck  mtanzania pekee anayeshiriki shindanoo la biashara duniani nchini German .
Mpaka sasa Deo Polycarp Goodluck anaongoza kwa kura chache sana huku raia kutoka BURUNDI ambaye yupo namba 2 akipambana kufa na kupona kushika namba 1,Tunahitaji  kura zenu  kuhakikisha Deo Polycarp Goodluck anabaki namba 1......Kumbuka shindano linaisha mwishoni mwa mwezi huu,sisi watanzania  ndio  tunaweza  kumpa  ushindi  mtanzania mwenzetu kwahiyo  tuendelee  kumpigia  kura  huyu  mtanzania  ,
 
JINSI YA KUPIGA KURA
1. Ingia kwenye link hii => https://www.entrepreneurship-campus.org/ideas/10/2994/
2. Shuka mpaka mwisho wa maelezo na picha utakuta maneno/namba maalum unazotakiwa uziandike, andika namba/maneno yanayoonekan kwenye kabox kadogo juu ya Button ya vote.
3. Utabonyeza button iliyoandikwa VOTE NOW, Hapo utakuwa umempigia kura na kumuwezesha kuwa mshindi.
Mpigie kura Deo leo. Tanzania kwanza.!

Tuungane Kumuunga mkono Mheshimiwa Paul Makonda.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua kampeni ya usafi ya mkoa iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Kampeni  ya usafi ya  siku 90 inayobeba kauli mbiu “usijifanye mstaarabu kuwa mstaarabu” itaanza kesho (1/5/2016)  kwa lengo la  kuboresha hali ya usafi  katika  mitaa mbalimbali pamoja na  jiji la Dar es salaam kwa ujumla,  ambapo itasaidia kuzuia magonjwa ya mlipuko, na wakazi wa jiji hilo wamehamasishwa kushiriki kufanya usafi katika mitaa yao pamoja na maeneo mbalimbali na baadae washindi  kupatiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 100 kwa mitaa miwili itakayokuwa imeshinda, ambapo pia  Mkuu huyo wa mkoa aligawa vifaa vya usafi kwa wenyeviti wa mitaa kutoka wilaya zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke.

Bw. Makonda amesema kuanzia sasa wakazi wa jiji la Dar es salaam watafanya usafi katika mitaa na maeneo yao  kila siku ya jumamosi kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi, na baada ya siku 90 washindi wawili, ambapo  mtaa utakaokuwa msafi na wenye makazi yaliyo katika mpangilio mzuri utapata zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 50 na mtaa utakaokuwa msafi lakini hauna makazi yaliyo katika mpangilio mzuri nao utapata fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 50, vilevile  mtaa utakaoongoza kwa uchafu utatangazwa ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wake kueleza namna ambavyo ameshindwa  kusimamia usafi katika eneo lake.

Paul Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa na Naseeb Abdul “Diamond  Platnumz ” Simba, Babu Tale, Ruge Mutahaba wa  Clouds Fm  na wengine wengi wakishiriki Kampeni ya  Usafi Leo Dar ya Makonda. (Picha na Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog)

“Mganga Mkuu wa Mkoa atafanya ukaguzi na kutangaza  vigezo vya washindi baada ya siku 90, tangu kuanza kwa kampeni hii, tunataka kuona mabadiliko na watu lazima washiriki kwa usafi na kuyapaka rangi  majengo yao. Suala la usafi si la Serikali pekee ni letu sote” alisema Makonda.

Aidha, ameagiza wamiliki wa vyombo vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es Salaam hasa daladala kuwa na vifaa vya kutupia taka katika vyombo vyao na kuanzia mei 2, atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa kampuni, taasisi na watu mbalimbali kuunga mkono zoezi hilo kwa kutoa misaada mbalimbali ikiemo kuhamasisha wananchi juu ya suala hili. Pia amewapongeza wakazi wa mkoa huo kwa kushiriki kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni ya usafi na  kuzipongeza  kampuni za Clouds Media group, Azam na redio ya EFM kwa michango yao katika kufanikisha kampeni hiyo ya usafi kwa mkoa wa Dar es salaam.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi, amewasisitiza wakazi wa  mkoa  wa Dar es salaam kufanya zoezi la usafi kuwa endelevu kwa kuwa wananchi wenyewe ndio wazalishaji wakubwa wa uchafu hivyo ni lazima wahahikishe wanauondoa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda (wa pili kushoto),akiwa sambamba na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa za Wilaya ya Kinondoni,Ilala pamoja na Temeke wakishiriki kwa pamoja kufagia ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Mh Paul Makonda kuzindua kampeni ya Usafi wa jiji la Dar Es Salaam,uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika mapema leo asubuhi Katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali serikali,dini na makundi mengine yakiwemo makundi ya michezo na waendesha boda boda.Mkuu wa Mkoa alizindua kampeni hiyo ya Usafi kwa kuwakabidhi Wenyeviti hao kila mmoja ufagio wa ajili ya kwenda kuwahamasisha wananchi wao katika mitaa yao.
Naye, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Bw. Mustafa Mkama, amesema wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaunga mkono kampeni hii na kuitaka jamii kwa ujumla ibadilike kwa kufanya usafi na Serikali nayo ihakikishe inaweka vyombo vya kuhifadhia taka  katika maeneo mbalimbali, sambamba na kuendelea kuelimisha wananchi umuhimu wa kuwa na  mazingira safi.

Uzinduzi wa kampeni ya usafi ya mkoa  wa Dar es Salaam ulitanguliwa na maandamano ya Mkuu wa Mkoa, viongozi mbalimbali wa dini na vyama vya siasa, wasanii mbalimbali akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul maarufu kama Diamond platnamz pamoja na wakazi wa mkoa huo, ambayo yalianza   katika wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni  na kuishia katika viwanja vya Leaders.

Ikumbukwe  kuwa 9 desemba 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli alihairisha shamrashamra za sherehe za Muungano na kufanya usafi, huku akiwataka watanzania wote kushiki kufanya usafi katika maeneo yao na kuagiza kuwa zoezi la kufanya usafi kuwa endelevu nchi nzima.

Angalizo
Naomba vijana wote watakokuwa tayari kushiriki kufanya usafi katika sehemu mbalimbali za jiji letu ,tuwasiliane kupitia:
Simu namba : 0625934656
Barua Pepe   : hassanmohamedtoziri@gmail.com


MAVAZI YANAVYOATHIRI MUONEKANO WA MTU.




Muhimu kutambua mavazi ni njia kubwa na nzuri ya kutambulisha tabia ya Mtu. Wengi wanapendwa au wanachukiwa kutokana na mavazi wanayovaa. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na heshima ama kwa kuwa mafupi au yamekuwa yakiacha sehemu kubwa ya kifua kuwa wazi.
Wasichana wa sasa wanaona kuvaa nguo zinazoacha wazi sehemu kubwa ya matiti kama fasheni.
Kuna mavazi ya aina nyingi ambapo yakivaliwa humfanya mtu apendeze au achukize. Uvaaji wa nguo unatakiwa kuzingatia umri na rangi ya mwili na pia mazingira ya nguo inapovaliwa.
Sio kila nguo ni ya kuvaliwa mchana na sio kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina nyingine za nguo hazistahili kuvaliwa barabarani unapotoka tu barabarani unaanza kupigiwa miluzi hiyo si sawa sawa.
Mathalani wewe ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaaje, kujiweka mrembo na mtanashati ni kitu muhimu. Siku hizi kuna mitimbo mbalimbali ya nguo za madukani, kushona mitindo ya kutumia vitenge, vitambaa kwa mitindo ambayo inatunza heshima ya mvaaji.
Unatakiwa kuvaa kulingana na mahali na wakati kwani kuna nguo za kazini na za kutokea lakini sasa hivi si ajabu ukakutana na mtu mchana wa jua kali akiwa amevaa nguo ya usiku au kumkuta akiwa amevaa viatu virefu huku akijua fika anatembea kwa miguu kwa umbali mrefu.

IFAHAMU SABUNI YA KURUDUSHA BIKRA.

Miongoni mwa maneno yaliyokwenye sabuni za kunawia ukeni.

 KUWA mrembo ni pamoja na kujikubali jinsi ulivyo na jinsi utakavyojiweka soap soapHata mtu akikupenda akupende  jinsi ulivyo. Pamoja na hayo kumekuwa na mambo mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya wanawake au wasichana kwa lengo la kufanikisha azma mbalimbali.
Miongoni mwa mambo hayo ni matumizi ya madawa mbalimbali ikiwemo yake ya kuongeza hips, makalio, kubadilisha rangi ya ngozi na hata kufanyia operesheni sura ili kuwa na muonekano ambao wanauona bora zaidi.
Pia kumekuwa na aina mbalimbali za sabuni kutoka ndani na nje ya nchi ambazo zimekuwa zikiuzwa ambazo zinadaiwa hurejesha ubikira zimesambaa sana madukani huku wateja wakubwa wakiwa ni wasichna na wanawake.

Hata hivyo walaatalam mbalimbali wanasema kuwa sabuni hhizo ambazo hutummika kwa kunawia sehemu za siti husaidia kurudisha bikira kwa mwanamke na hata kuwa na mnato.
Lakini wanaootumia sabuni hizo wameonywa kuwa  sabuni hizo zina kemikali zenye madhara makubwa kwa mtumiaji kwani zina uwezo mkubwa wa kusababisha kansa ya shingo ya kizazi.
Kwa mujibu wa Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka anasema hivi sasa kumekuwa na sabuni mbalimbali ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli.
Mtaalam huyo Anasema  Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji  yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano  kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa.
Pia michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi. Sabuni hizo zinatengeneza hali fulani ukeni  lakini haiwezi kurejesha hali ya maumbile iliyopotea.
Mfamasia huyo anasema wanaotumia sabuni hizo wako katika hatari kubwa ya kuambukuzwa magonjwa na hata kupata saratanni ya shingo a usazi kwani kemikali zinazotumika katika kutengeneza sabuni hizo zina athari kubwa kiafya.
Anataka wanawake kutatambua thamani yao na kuachana na matumizi ya sabuni hizo ambazo hazina manufaa yoyote na badala yake zimekuwa na madhara makubwa kwao.
Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Dodoma, Fredrick  Luyangi  anasema mrudiano wa athari hasa kwa matumizi ya sabuni huleta athari kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa taratibu bila mhusika kufahamu.Sabuni hizo husababisha kansa ya kizazi na kubainisha sabuni hizo licha kupigwa marufuku zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka ya vipodozi.
“Mara nyingi kwenye operesheni zinazofanyika zimekuwa zikiondolewa sokoni lakini hata hivyo zimekuwa zikiingizwa kwa wingi hali inayofanya zoezi la kudhibiti kuwa gumu” anasema.
Anawataka wanawake kuacha matumizi ya sabuni hizo ambazo zina madhara makubwa sana kwao kwani zikikosa wanunuzi zitaondoka sokoni.



USAFI KIPINDI CHA UJAUZITO.



Kipindi cha ujauzito wanawake wengi hujikuta wakiacha kuzingatia hatua mbalimbali za kujitunza ili kubaki warembo, matokeo yake hupoteza mvuto.

Hali hiyo inaweza kuendelea hata baada ya kujifungua na huenda ikawa mbaya zaidi kwa kuwa mara nyingi kipindi hicho mama hujikuta akitumia muda mwingi kumwangalia mtoto.

Kujifungua au ujauzito haiwezi kuwa sababu ya mwanamke kupoteza urembo uliokuwanao awali. Hivyo ni jukumu la mwanamke mjamzito au aliyejifungua kuhakikisha anabaki na mvuto wake ukiwa kwenye kiwango stahiki.

Kuwa mrembo siyo lazima upake vipodozi vyenye kemikali kwani vinaweza kumsababishia madhara mtoto kwa kuwa atatumia muda mrefu akiwa mwilini kwako.

Katika kipindi hiki mama mjamzito au aliyejifungua anatakiwa kuepuka kupaka mafuta, losheni au manukato yenye harufu kali inayoweza kuwa na madhara kwa mtoto hata kumsabishia wakati mgumu katika kupumua.

Ni vyema utumie vipodozi visivyo na kemikali ili kujilinda usipoteze mvuto wako. Pia tumia muda mwingi kufanya mazoezi mepesi yatakayoweza kukusadia kutengeneza umbile (shape), yako na kuifanya ionekane yenye mvuto wa hali ya juu hata ikiwa umetoka kujifungua.

Hakikisha pia kucha zako zinakuwa fupi na safi, hii haimaanishi kwamba huruhusiwi kupaka rangi unaweza kuziremba kwa mtindo wowote unaopenda lakini ziwe katika kiwango ambacho hakitamdhuru mtoto kwa namna yoyote.

Kitu muhimu cha kuzingatia katika kipindi hicho ni usafi na mwonekano wa ndani na nje. Kwa kufanya hivyo, hata mtoto atakuwa katika mazingira salama yanaweza kumtamanisha mtu mwingine kutaka kumshika.

MFAHAMU CHERELLE CAMPBELL




Mwanamke mmoja mwenye makazi yake campbel, Uingereza amejikuta anaingia katika wakati mgumu baada ya kufanya upasuaji wa urembo kwa lengo la kutengeneza kibonyo shavuni.

Mwanamke huyo Cherelle Campbell, ambaye ni mwanasheria mtarajiwa, alikuwa mwanamke wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa urembo kutengeneza kibonyo.

Upasuaji huo wa urembo unahusisha kutengenezwa kw amatundu kadhaa shavyuni kutengeneza muonekano wa kibonyo mtu anapotabasamu au kuongea.

Shughuli hiyo yenye gharama  ya dola za Marekani 2,500 imeletea shida binti huyo ambaye anasema kwamba sasa anajiona kama kituko, kwani matundu yameingia ndani zaidi.

ASALI KATIKA UREMBO WAKO



Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni daktari, Amy Wechsler anasema hali ya kunyunyurika iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiliwe n vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.

 Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili pia.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya maji  kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu a ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.

Mimi nakushauri jaribu moisturizing ya asali ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha na kutatarika.

Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziwa.
Kisha pasha moto mchanganyiko huo, kisha paka mchanganyiko huo katika uso wako na kupumzika kwa dakika kama kumi hivi.
Kisha jioshe kwa maji ya vuguvugu.Kama unataka kitu kama kosmetiki agiza lotion ya asali ili kuweka sawa ngozi yako.
Hakikisha unanunua lotion ambayo imetengenezwa kwa asali isiyochujwa.
Aina zote za asali zinasaidia kuondoa mikunjo ya uzeeni.

MAYAI YA KWARE SASA NI KIKOMBE CHA LOLIONDO


Hivi sasa kumeibuka tiba ya ‘mayai ya kwale’ ambayo inavuma kila kona na imekuwa gumzo kila mahali. Tiba hii ni ya kimaajabu kwani uvumi uliopo ni kwamba mayai ya kwale yana uwezo wa kutibu magonjwa yote sugu.
Kasi ya kushauri wagonjwa na hata wasio wagonjwa kutumia mayai haya badala ya kwenda hospitali kwa uchunguzi wa afya zao inaongezeka na maelekezo yanayopatikana mitaani juu ya kutumia tiba hii ni ya ajabu na yanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Nilishuhudia mtu mmoja akimwelekeza mgonjwa kuwa alipaswa kuyapasua mayai na kuyapondaponda pamoja na magamba yake na kisha ayanywe katika hali ya ubichi. Mwingine aliambiwa ayapasue na kisha ayakoroge pamoja na asali au maziwa kisha anywe, wengine wanaelekezwa kuyachemsha kama mayai ya kawaida na kisha kula kiini cha ndani. Uvumi huu unaenea kwa kasi mitaani.
Kutokana na kuvuma kwa tiba hii, mayai haya hivi sasa yanaonekana kusakwa kila mahali na yanauzwa kati ya Sh15,000 hadi 20,000 kwa trei.
Uvumi wa tiba hii hauna tofauti na ule uliozuka nchini juu tiba maarufu kama ‘kikombe cha Babu’. Watu wengi walikatisha matibabu kwenye hospitali mbalimbali na kuamua kwenda Kijiji cha Samunge kwenda kupata kikombe cha babu na kufanya kuwe na misururu mirefu ya watu waliokesha usiku na mchana. Hii ilizusha adha kubwa hasa kutokana na kutokuwepo na maandalizi ya vyoo hivyo watu kujisaidia ovyo vichakani.
Adha ya safari ndefu na kukaa kwenye foleni kwa zaidi ya siku tatu, kulifanya wenye afya mbaya kushindwa kuhimili na hata kupoteza maisha.
Katika mazingira haya ya kuibuka tiba za ajabuajabu ambazo hazijathibitishwa kitaalamu, ni vyema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikatoa ufafanuzi.
Isisubiri hadi watu wapoteze maisha halafu ndiyo ianze kuja na maelekezo tena yanayopingana na yale ambayo jamii inaamini. Kuchelewa kunafanya wengi wapoteze fedha na hata kuacha tiba sahihi na kukimbilia kitu ambacho kinavumishwa tu.
Serikali haipaswi kukaa kimya wakati watu wakiendelea kutibiana kwa vitu ambavyo havijathibitishwa kitaalamu.Kama Serikali ingechukua hatua mapema, watu wasingepoteza maisha kupitia kikombe cha babu.
Uvumi huu wa tiba ya mayai ya kwale hauna tofauti na Kikombe cha Babu.
Katika ulimwengu huu wa utandawazi na soko huria, ni kawaida kusikia mambo mapya yakiibuka kila kukicha, lakini kama mambo hayo yanagusa afya zetu, hatuna budi kuwa makini na waangalifu zaidi.

Wakili Kenya na moango wa kuwa mkwe wa Obama



Taarifa kuwa wakili mmoja wa kenya amesema yuko tayari kutoa mahari kwa mtoto wa raisi wa Marekani,Barrack Obama zimeenea duniani kote Felix Kiprono amesema yuko tayari kutoa ng'ombe 50,kondoo 70 na mbuzi 30 kwa ajili ya mahari ya mtoto wa Obama,Malia Obama.Hivyo anajiandaa kuzungumzia swala hilo na baba wa mtoto huyo atakapo tembelea Kenya ,mwezi Julai.

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh atangaza kuipindua Burundi.




Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinwa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo alitimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''

Umuhimu wa kukojoa baada ya tendo la ndoa.



Mara nyingi tunashauriwa kukojoa kila baada ya tendo la ndoa. Japokuwa wanawake wengi pamoja na kuwa na hamu ya kwenda haja ndogo kila baada ya tendo ila kutokana na uvivu na uchovu ujikuta katika usingizi mzito na kusahau tendo hili muhimu baada ya kufika kileleni. Umuhimu wa tendo hili ni kupunguza na kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa ya njia ya mkojo(U.T.I) na magonjwa ya zinaa(S.T.I)

Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa huongeza presha kwenye kibofu na kusababisha hamu ya kukojoa kila baada ya tendo hali inayokuwezesha kuondoa vimelea vya magonjwa mbali mbali kabla ya kusambaa kwenye kibofu na sehemu nyingine za mwili kusababisha matatizo makubwa. kwa wanaotumia kondomo pia unashauriwa kufanya hivo endapo itapasuka sambamba na kusafisha sehemu za uke na uume kwa maji safi na sabuni.
kwa wanaofanya mapenzi ya mdomo(chumvini na kulamba kone) unashauriwa kutoingiza shahawa, maji maji ya uke/ume na damu mdomoni kwani kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ukimwi na hepatitis B.

MSIBA CCM:Kifo cha Kapteni Komba kimeacha pengo.



Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia leo alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .

Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.

Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa mahututi .

"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk Ishan

Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.


watuhumiwa wa ugaidi walipopandishwa kizimbani.


Na Mpenda Mvula,Songea.
WATU saba wanaodaiwa kuunda mtandao wa kigaidi Songea mkoani Ruvuma wameshakamatwa na muda wowote kuanzia sasa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowabili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa wanadaiwa kuhusika na matukio matatu tofauti ya urushwaji na utegaji wa mabomu ya kienyeji.

Alifafanuwa kuwa tukio la kwanza lilitokea Septemba 16 mwaka jana majira ya saa 1.30 jioni huko katika eneo la Misufini kikundi hicho kinachojihusisha na ugaidi kiliwarushia Askari polisi waliokuwa doria bomu la kienyeji la kurushwa ambalo liliwasababishia askari watatu kujeruhiwa.

Alisema kuwa katika tukio lingine ambalo lilitokea Oktoba 27 mwaka jana majira ya saa 10 jioni lilichimbiwa ardhini bomu katika eneo la Mshangano ambalo hutumiwa kama kituo cha ukaguzi wa magari yanayotoka na kuingia Songea mjini na askari wa kikosi cha usalama barabarani kando kando mwa Barabara inayotoka Songea kwenda Njombe kwa lengo la kuwalipua askari wa kikosi hicho.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kuwa pia kabla hawajatimiza hazma hiyo askari wa usalama barabarani waliokuwa kwenye eneo hilo waliligunduwa bomu hilo likiwa limechimbiwa ardhini na jeshi la polisi kwa kushilikiana na jeshi la wananchi (JWTZ) baada ya kupata taarifa hiyo walifika kwenye eneo la tukio na waliweza kuliteguwa bila kuleta madhara.

Alilitaja tukio lingine la tatu kuwa lilitokea Disemba 25 mwaka jana majira ya 1.30 usiku katika eneo la Majengo Kotazi kikundi hicho cha ugaidi pia kilidhamilia kuwarushia bomu askari waliokuwa wanafanya doria ambapo mtu mmoja kutoka katika kikundi hicho alijaribu kuwarushia bomu askari hao na kabla hajarirusha lilimlipukia yeye mwenyewe na kufariki Dunia papo hapo na kusababisha askari polisa wawili kujeruhiwa vibaya.

Alieleza zaidi kuwa timu ya upelelezi toka ndani ya jeshi la Polisi kwakushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimeweza kubaini eneo linalotumika kwa mafunzo ya kigaidi na kikundi hicho na kwamba mpaka sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo na wanatarajia kupanda mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Baba atuhumiwa kwa kumfanyia ukatili wa kutisha mtoto wa ndugu yake.



Baba mkubwa aliyetajwa kwa jina la Mohamed Said a.k.a Muddy, mkazi wa Tegeta-Msufini jijini Dar amepigwa pingu akituhumiwa kumfanyia ukatili wa kutisha wa kumsulubu mtoto wa kiume wa mdogo wake, mwenye umri wa miaka 6( jina linahifadhiwa). 

Inadaiwa kuwa Muddy alimchukua mtoto huyo kutoka kwa wazazi wake wanaoishi mkoani Mtwara kwa lengo la kuja naye Dar kwa ajili ya kumsomesha lakini kinyume na lengo hilo, jamaa huyo alipomfikisha Dar ilidaiwa alianza kumfanyia ukatili mtoto huyo wa dozi ya vipigo. 

Majirani walisema kuwa jamaa huyo amekuwa akimshushia kipigo mtoto huyo mara kwa mara kwa kutumia bomba la plastiki na waya wa umeme huku adhabu kama kumnyanyua miguu juu kichwa chini, kumnyanyua juu kwa kumshika masikio na kushinda muda mrefu bila kula vikiwa ni sehemu ya maisha ya mtoto huyo.

KUHUSU UTEKAJI WA VITUO BYA POLISI : LEMA ATOA TAMKO.


Wakati Jeshi la Polisi likiwa kwenye operesheni ya kuwasaka watu wanaovamia, kuteka vituo vya polisi na kupora silaha, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amemgeukia Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja, akisema anahusika katika kupanga mkakati wa kutekeleza vitendo hivyo vya uhalifu.

Amesema mkakati huo umepangwa na Kamishna Chagonja kwa nia mbaya ya kumhujumu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, ili kuchafua taswira ya uongozi wake mbele ya macho ya jamii.

Lema alisema hayo wakati akichangia mjadala kuhusu taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe, bungeni juzi.

Alisema kutokana na nchi kufikia kuwa mithili ya 'gheto', ambamo kila anayeishi humo ana uhuru wa kufanya anavyotaka, katika Jeshi la Polisi, Chagonja haamini kama Rais Jakaya Kikwete amekwishafanya uteuzi wa IGP na hivyo, kujiamulia kufanya mambo anavyotaka.

Lema alisema hali hiyo ni uthibitisho dhahiri wa taarifa alizonazo kwamba, jeshi hilo limepasuka vipande viwili, ambavyo kila upande unafanya unavyotaka.

"Na mimi nikiwaambia na nimelichunguza. Jeshi la Polisi limepasuka. Ma-RPC (makamanda wa polisi wa mkoa) wanalalamika. Chagonja haamini kama Rais ameshafanya uteuzi wa IGP," alisema Lema.

Aliongeza: "Na mimi nasema hata hizi bunduki zinaoibwa inaweza ikawa mkakati wa Chagonja ku-subotege (kumhujumu) IGP."

Alisema hata Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, pamoja na watu wote duniani wanaujua mkakati huo wa Chagonja, lakini wote wanashindwa kupaza sauti kuueleza.

"Hii nchi ni kama gheto, yaani nchi ni kama gheto kabisa. Hujui serikali iko wapi. Na tukiongea humu kuwashawishi wananchi wawe imara tunasemwa tunachochea vurugu," alisema Lema.

VURUGU ZAIBUKA KUHUSU LIPUMBA KUPIGWA NA POLISI.




Mbatia alisimama na kutoa hoja ya dharura ijadiliwe Bungeni kuhusu Polisi Dar es Salaam kutumia nguvu dhidi ya wanachama wa CUF na kuwapiga.

Mbatia: "Nimesikitishwa sana, Lipumba amepigwa, watoto wamepigwa mabomu, waandishi wa habari wamepigwa, na Polisi wakasema wamepewa maagizo"

Mbatia: "Prof Lipumba ni Mwenyekiti wa chama chenye wabunge zaidi ya 30 na Mwenyekiti wa chama kinachoshiriki serikali ya Zanzibar, sasa kama yeye anafanyiwa hivi itakuwaje Wananchi wa kawaida?"

Mbatia: "Naomba kutoa hoja Bunge liahirishe shughuli zake ili tujadili tatizo hili lililotokea"
Lakini Spika Anna Makinda aliipinga hoja yake na kusema,

Spika Makinda: "Naiagiza serikali iandae taarifa kamili, kesho ilete humu Bungeni, ndipo nitaruhusu hoja hii ijadiliwe, Sasa Hapana".

Spika Makinda: "Someni kanuni vizuri, zinaniruhusu kuamua kama kadri ninavyoona, hoja za namna hii haziungwi mkono"

Hilo likazua tatizo baada ya Baadhi ya wabunge wengi wa upinzani kugoma kuendelea na ratiba, wanataka ijadiliwe sasa, wanapiga kelele, kuna hali ya taharuki.
Spika Makinda akaamua kusitisha shughuli za Bunge hadi saa 10:00 jioni kutoa nafasi ya makubaliano kuhusiana na suala hilo

Auwawa na mwiliwake kutundikwa juu ya mti soma zaidi hapa

WATU wawili wameuawa katika matukio tofauti, akiwemo kijana mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi yake.
Kijana huyo alikutwa amenyongwa na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutundikwa juu ya mti kwa kutumia suruali aliyokuwa amevaa katika kijiji cha Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Longinus Tibishubwamu alisema tukio hilo limetokea Januari 27, mwaka huu. Alisema mwili ulikutwa na jeraha kwenye mguu wa kulia na uchunguzi wa daktari unaonesha kuwa kijana huyo aliumia kabla ya kunyongwa shingo na chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana.

Wakati huo huo, Kamanda Tibishubwamu alisema mwanamke asiyefahamika jina wala makazi yake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30 ameuawa kisha mwili wake kuwekwa chini ya daraja dogo lililopo katika kitongoji cha Jihingu kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu umekutwa ukiwa na majeraha kichwani, usoni na ubavuni na kwamba Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi juu ya mauaji hayo ili kuwabaini na kuwakamata wahusika.

Profesa Muhongo ajiuzuru kujiosha.



Kufuatia kuhusishwa na sakata la uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameamua kumuandikia barua Raisi ya kujiuzulu wadhifa wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo ameelezea furaha yake ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika wizara yake kwa kipindi chake akisema kuwa nidhamu na uwajibikaji vilikuwa dira ya maendeleo wizarani hapo.

Profesa Muhongo amekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa anaamini kujiuzuru kwake kutaisaidia Serikali na Bunge kutuliza malumbano ya Sakata hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Amesema yeye si mwizi na hawezi kuuza utu wake kwa kupewa rushwa ili kuwakandamiza watanzania.

“Nimeamua kujiuzuru kwa dhati kabisa bila kushinikizwa na mtu yeyeote, inaonekana mimi ndiyo nitamaliza mjadala huu wa sakata la Escrow, tuna mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kujadiliwa lakini watu wamekazana na Escrow, nimemuandikia Rais barua rasmi ya kujiuzuru wadhifa wangu, amesema Profesa Muhongo.

Amesema pamoja na kujiuzuru anatarajia mapema kuzungumza na watanzania ili kuwaeleza ukweli wa sakata la Escrow na kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa Tanzania na watu wake.

Amesema yeye amelelewa katika malezi yenye maadili mema na kwamba tokea alipomaliza masomo yake aliaswa kutopokea ama kutotoa rushwa hivyo hawezi akapokea rushwa kwa ajili ya kuutukana utu wa mtanzania hicho ndicho kinachomgharimu.

WALIOMCHINJA KATIBU WA CCM HUKO KAHAMA,WAKAMATWA,NI KUNDI LA WACHINJA WATU,YUMO DIWANI WA CCM


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kunasa mtandao wa watu wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya watu kwa kuchinja kwa visu,ikiwemo tukio la mauaji ya Katibu wa Chama Chama Mapinduzi kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga Daudi Lusalula Mbatiro(56) aliyeuawa kwa kuchinjwa kama kuku mwaka jana kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa Tukio la kuuawa kwa katibu huyo wa CCM lilitokea Desemba 5,2014 saa mbili usiku wakati katibu huyo wa CCM kata ya Mwaluguru ambaye pia alikuwa ni katibu wa elimu,malezi na mazingira baraza la wazazi wa CCM wilaya ya Kahama akitokea kata ya Kagongwa kwenda nyumbani kwake Sungamile baada ya kutoka kwenye mkutano wa chama chake uliokuwa unafanyika mjini Kahama. Waliotajwa na jeshi la polisi kuhusika katika mtandao huo ni pamoja na diwani wa kata ya Mwalugulu wilayani Kahama Bundala Kadilanha(CCM),mfanyabiashara wa Kagongwa Tobo Mwanasana,pamoja na Emmanuel Maziku,Masanja Shepa,Samwel Seni Budugu na Shija Shepa. Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alisema katika uchunguzi wa mauaji ya katibu wa CCM kata ya Mwalugulu Daudi Mbatiro jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa Emmanuel Maziku na Masanja Shepa na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na mauaji hayo. Alisema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao wawili,waliwataja wahusika wengine ambao ni Bundala Kadilanha(diwani wa Mwalugulu),Tobo Mwanasana(mfanyabiashara,Samweli Seni Budugu mkazi wa Mwakitolyo na Shija Shepa mkazi wa Mwalumba Kahama. Alisema awali jeshi la polisi baada ya kupata taarifa za watu hao liliweka mtego kwa kuwapigia simu ili kuwakodi kufanya mauaji katika kijiji cha Nyindu na kufanikisha kuwakamata watu hao ambao hujihusisha na matukio mbalimbali ya mauaji. Alisema baada ya kuwafanyia mahojiano watu hao wawili walikiri kuhusika na matukio ya mauaji katika mkoa wa Shinyanga na Tabora kwa kukodiwa ili kuchinja watu kwa kisu na wao sio wakata mapanga ingawa wanaua vikongwe na kulipiza kisasi. Kamanda Kamugisha alisema watuhumiwa walisema kiongozi wao ni Samweli Seni Budugu na wenzake ni Tobo Mwanasana,Bundala Kadila na Shija Shepa na kabla ya mauaji hayo wanaenda kupakwa dawa kwa waganga wao wa jadi ambao ni John Shija mkazi wa kijiji cha Lyabukande na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Tabu mkazi wa Kizungu. Kamanda Kamugisha alisema watuhumiwa wote wamekiri kuhusika na matukio ya mauaji ya marehemu Ngolo Sakumi(69) mkazi wa Mwalugulu na walikodiwa kwa shilingi 1,000,000/= aliyewakodi ni Jikuba Kajile na Lukuba Nangi. Tukio jingine walilokiri kuhusika ni mauaji ya Mary Seleman Masenya(45) mkazi wa kijiji cha Matinje na walikodiwa kwa shilingi 800,000/= na wanawake watatu ambao ni wake wenza wa marehemu. Alitaja tuko jingine walilohusika ni lile la mauaji ya Mboje Seni(70) mkazi wa kijiji cha Butondo na walikodiwa kwa shilingi 800,000/= walikodiwa na Mwanabundi mkazi wa Butondo na tukio jingine ni mauaji ya Kwigema Lubinza(60) mkazi wa kijiji cha Kakulu kata ya Nyahanga. Kamanda huyo alisem jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwakamata wahusika wengine wa matukio hayo ikiwa ni pamoja na waganga wa kienyeji waliohusika huku akiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wote wa mauaji ya kukodiwa na mauaji ya vikongwe ili kukomesha kabisa mauaji hayo.
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency