Home » » Sehemu ya kwanza:Mr Chande,Kiongozi mkubwa wa Freemason kutoka Afrika Mashariki akizungumzia yanayowahusu.

Sehemu ya kwanza:Mr Chande,Kiongozi mkubwa wa Freemason kutoka Afrika Mashariki akizungumzia yanayowahusu.

 
Mtanzania mmoja, ambaye alianzia ngazi ya chini hadi kufikia kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki, akiongoza zaidi ya vitengo 50, anaeleza kwa undani namna alivyojiunga na chama hicho akiwa bado kijana. Akiwa na umri wa miaka 24, Jayantilal Keshvji Chande, maarufu zaidi kwa jina la Sir Chande, alikuwa tayari ameshavutiwa kujiunga na Freemason, lakini hakujua vipi na wapi kwa kuanzia.

Kwa maneno yake, Sir Chande anasema kuwa hamu ya kujiunga na Freemason ilichochewa na tabia ya rafiki zake wawili wa wakati huo, Mwingereza, Bob Campbell Ritchie na John McLean kutoka Scotland.

Rafiki zake hao walikuwa na ratiba isiyokuwa ya kawaida hasa wakati wa jioni. Kila Jumatatu baada ya kutoka kazini, walikuwa wakihudhuria kile alichokiita ‘vikao vya kushangaza’ kwenye jengo moja lililopo karibu na bahari, Dar es Salaam.

Taratibu, udadisi wa Sir Chande kuhusu sehemu waliyokuwa wakienda rafiki zake ikajulikana, baada ya wao wenyewe kumweleza kuwa walikuwa ni wanachama wa Freemason.

‘Haraka nilitaka kuwa mwanachama’, anaandika Sir Chande katika kitabu chake “Usiku Afrika; Njia kutoka Bukene.” Kwa kuwa kujiunga Freemason siyo kwa kutuma maombi au kwa usaili, bali kwa kupendekezwa, haikuwepo njia nyingine ya kufanya hivyo.

Marafiki zake Sir Chande walimtambulisha kwa wanachama wa Freemason wengine, Sheikh Mustafa na Jivraj Patel, ambao kwa mwanzoni walilazimika kuwa kama ndugu yao kwa kuwa walikuwa wakifahamika ndani ya chama hicho.

Ilimchukua Sir Chande miaka miwili ya kusubiri, kuchunguzwa na kuona kama alikuwa na uadilifu unaohitajika kujiunga katika chama hicho, kinachodaiwa kujihusisha na giza na siri ikiwamo matambiko na kutoa kafara za binadamu kupata utajiri na nguvu.

“Kama ambavyo nilitarajia,” anaandika Sir Chande akieleza: “Nilitakiwa kusubiri kwa miaka miwili wakati naangaliwa kama ninaweza kufaa.”

“Hakuna mtu ambaye alinionya kuhusu maumivu anayoyapata mtu wakati wa kipindi cha matazamio, bila kujali masuala ya kifedha au msimamo wake kwenye jamii,” anaandika.

Kwa mujibu wa Sir Chande, wakati wa kuchunguzwa, kazi zake zote za kila siku, ndani na nje ya ofisi zilikuwa zikifuatiliwa kwa umakini mkubwa. Baadhi ya rafiki na ndugu zake pia walihojiwa.

“Ingawa nilikuwa natoka katika familia za watu wenye asili ya Asia waliofanikiwa kibiashara Afrika Mashariki, haikusaidia kurahisisha,” anaandika na kuongeza kuwa baada ya miaka miwili alijiunga na moja ya taasisi hatari duniani.

Kujiunga Freemason siyo kwa kuomba au kusailiwa tu. Kinyume na wengi wanavyodhani, badala yake kwa mujibu wa Sir Chande, mtu anakuwa mwanachama kwa kupendekezwa na mtu ambaye tayari ni mwanachama.

Itaendelea Jumanne ,fatilia ujue ukweli kuhusu tuhuma za kuabudu mashetani na kama kweli Freemason ni taasisi ya siri.

Usisahau pia kututumia maoni ama ushauri kupitia mawasiliano yetu.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency