Katika makubaliano hayo ya kugawana mamlaka Ashraf Ghani ndio rais mpya huku mpinzani wake Abdullah Abdullah akimchagua afisa mkuu atakayekuwa na mamlaka kama yale ya waziri mkuu.
Ashraf Ghani atakuwa rais mpya mwenye mamlaka mengi na makubaliano hayo yanasema kuwa afisa mkuu atakayechaguliwa atakuwa akiwajibika kwake.
Hata hivyo bwana Ghani amepoteza harakati za kutaka kutawazwa baada ya matokeo ya uchaguzi.
Wawili hao wametia sahihi makubaliano ya kubuni serikali ya kitaifa kabla ya matokeo hayo ya uchaguzi kutangazwa.Na afisa mkuu atakayechaguliwa na Abdulla Abdullla atakuwa sako kwa bako na rais wakati atakapotawazwa.
Bwana Abdullah alikabidhiwa uwezo wa kuwateua maafisa wengine wa ngazi za juu dhidi ya Ghani.Makubaliano hayo yanasema kuwa makundi hayo mawili yatashirikishwa vilivyo katika uongozi wa taifa hilo.
Hata hivyo hakutakuwa na usawa wa kuwateua maafisa zaidi katika ngazi za chini za serikali swala ambalo huenda likazua ubishi mkubwa.Lakini baada ya mgogoro mkubwa wa kampeni za uchaguzi wa miezi kadhaa,udhabiti wa taifa hilo haujulikani.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO