Home » » Habari Kamili : Mashujaa bend yaitenda vibaya Tanzania Classic.

Habari Kamili : Mashujaa bend yaitenda vibaya Tanzania Classic.

Hichi ndio walichofanyiwa Tanzania Classic  na bendi ya msiki ya mashujaa baada ya kupoteza muda na nafasi zao kuwapamba ili kunyakuwa tunzo za Kili Award.
Na hichi ndio walichoandika Tanzania Classic kupitia mtandao wa Facebook.
[HUU NDIYO USWAHILI WA TZ]
mwaka huu mwezi wa tano kulifanyika tuzo za kili music award katika tuzo hizo wanamziki mbalimbali walishindana kuwania tuzo hizo mfano mzuri katika upande wa mziki wa dansi kuna bendi kadhaa zilishiriki katika shindano hilo mfano wa Mashuja bendi ambayo ilibuka na tuzo nyingi katika tuzo hizo,
Naweka kumbukumbu sawa kabla ya kufanyika tuzo hizo bendi mbalimbali zilifanya kampeni ya kuomba kura kwa mashabiki kupitia mitandao ya kujamii mfano facebook ili mashabiki waweze kuwapigia kura na kuibuka ushindi!!!!!Nakumbuka wakati wa kampeni hiyo nilijitolea bila kushawishiika na mtu yoyote kuwapigia kampeni mashujaa kwa nguvu zote kupitia mitandao ya kijamii mfano facebook , twitter, whatsupp ili waweze kuibuka washindi, Nakumbuka wakati huo tulijenga urafiki wa karibu sana na viongozi wa mashujaa maana wengine walikuwa wanapiga simu na kunipongeza.
Baada ya ushindi Mashuja walitoa ahadi mbalimbali kwanza walinihaidi kunipa kadi maalum ambayo nitakuwa naitumia kuingia kwenye shooo ZAO, Pia walitoa ahadi ya kuhakikisha wanashirikiana na mimi katika kuendeleza mtandao wangu wa www.tanzaniaclassic.com ili uweze kusonga mbele zaidi,Pia nilifikia hatua ya kukutana na mkurugenzi wa Mashujaa maarufu Papa Maisha tukapanga mikakati mbalimbli lakini cha kushangaza ahadi zao zote zilikuwa ni hewa kabisa maana zinaonekana zipo kiuswahili zaidi kwasababu mpaka sasa hakuna lililofanyika zaidi ya kutoa kauli za kiswahili ambazo hazina kichwa wala mguu na viongozi wengine hiyo bendi wakitoa kauli za dharau baada ya kujioana wamepata ushindi wa kunyakua tuzo,
Tatizo langu ni kwanini Mashujaa walitoa ahadi za uongo ?? Na je kulikuwa na ulazima gani kutoa ahadi ambazo hasitekelezeki ?? je kulikuwa na ulazima gani mkurugenzi wao papa Maisha kukutana na mimi kutoa ahadi za uongo? Je Papa Maisha haoni ni aibu kwa mtu mzima kama yeye kuendekeza uswahili usiyokuwa na faida yoyote katika mziki ??? Hakika hii tabia inabidi ikomeshwe mara moja kwasababu ndiyo inasababisha huu mziki udharauliwe na wadau kutokana na baadhi ya wamiliki wa bendi kuendekeza uswahili kipuuzi kama huu ambao mwisho wa siku unawakimbiza wadau ambao wangependa kusaidia mziki huu ili usonge mbele ,
Nina mengi ya kuongea ila nautaka uongozi mzima wa Mashuja bendi waache dharau bado wanasafari ndefu kwenye mziki kwasababu tabia ya kuendekeza uswahili haitawafikisha popotea zaidi inawashusha hadhi mbele ya jamiii, mimi binafsi niliwapenda Mashujaa na kuwa tayari kushirikiaana nao lakini nimegundua inaongozwa na watu wasiyokuwa na fadhira, watu wasiyokuwa na kumbukumbu juu ya mambo mazuri wanayofanyiwa na wadau ili kuendeleza bendi yao,
Narudia tena Mashujaa bendi acheni uswahili maana kwaa mtindo huu mziki huu utaendelea kuwa nyuma,
LikeLike ·  · 

Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency