Home » » Hatari ya mapenzi ya Facebook

Hatari ya mapenzi ya Facebook




Dada mmoja alikutana na kijana mmoja kwa njia ya facebook na wakapendana hapa mtandaoni.
Baada ya kuchati kwa muda mrefu wakaamua waende kuonana na hatimaye wakaona na binti kukaribishwa katika chumba alichopanga kijana huyo.
Alipofika akaanza kuhisi kuwa amefanya maamuzi yasiyo sahihi kwenda pale kwani chumba kilinuka harufu ya pombe na bangi na pia kulikuwa na vijana wengine wapatao wanne wakiwa wamelewa pale.
wakamwingilia kinguvu dada yule na kisha baada ya kugundua kapoteza fahamu wakamtupa nje karibu na barabara na dada alipopata fahamu kwa aibu akaondoka na hakumwambia mtu na kukaa kimya.
Miezi michache baadae akagundua kuwa ni mjamzito na kwa sheria za ile nchi akatakiwa kufukuzwa katika ile jamii kwani amefanya kosa la kuiabisha jamii kupata ujauzito bila muda wake muafaka kufikia.
Siku chache baadae ikaja onekana maiti yake ikiwa pembeni ya mji ule katika nyumba moja akiwa na karatasi mkononi iliyoandikwa:
" Kwa wadogo zangu miliobaki, mitandao ya kijamii ina faida kubwa na hasa zake pia... kamwe msiwe wepesi wa kufanya maamuzi na kuja kuwa wahanga wa matatizo niliyokumbana nayo mimi dada yenu.... Nawapenda sana"
Sala kwa ajili yako
Mitandao ya kijamii itakupa marafiki watao kupanua mawazo ya kuziboresha kazi zako na sio watakao kuharibia kazi zako na maisha yako pia.
Kila rafiki atakuwa hazina ya mafanikio yako nawe utapata busara na hekima ya kuwatambua marafiki feki na wale wenye nia njema

Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency