Home » » Baada ya Brazil kufungwa 7:Sakata la ROMA kuamia SHAROBARO rec

Baada ya Brazil kufungwa 7:Sakata la ROMA kuamia SHAROBARO rec


Kabla ya mechi ya jana ya Ujerumani na Brazil, rapper Roma Mkatoliki aliwaahidi mashabiki wake kuwa timu yake ya Brazil ikifungwa na Ujerumani atahama Tongwe Records na kwenda kufanya kazi Sharobaro Records inayomilikiwa na Bob Junior.

Kupitia ukurasa wa Facebook, Roma aliandika
                          " Brazil damu…no matter waat’ "
huku akiambatanisha na picha yenye ujumbe usemao
 ‘Kama Brazil tukifungwa leo nahama Tongwe Records naenda Sharobaro Records kwa Bob Junior’ 
Kauli hiyo imewafanya mashabiki wake kutaka kujua nini kinaendelea baada ya Brazil kupata mkong’oto wa bao 7-1.

Baada ya Roma kupigiwa simu kutaka kujua lini ataingia kwenye booth ya Sharobaro Recs na kujibu: "Masuala ya mpira sasa hivi sizungumzi, naomba niache, kama una mambo mengine tuzungumze.”
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency