Home » » Taarifa muhimu juu ya kuteketea kwa moto msikiti wa Mtambani.

Taarifa muhimu juu ya kuteketea kwa moto msikiti wa Mtambani.

Msikitini maarufu wa Mtambani ulioko Kinondoni, Dar es Salaam umeteketea kwa moto.Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo msikiti huo uliteketea kwa moto jana jioni na hakuna aliyejuruhiwa katika tukio hilo.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kwamba moto huo ulizuka ghafla baada ya Swala ya Magharibi na kuteketeza sehemu yote ya juu ya msikiti huo.
http://photos-d.ak.instagram.com/hphotos-ak-xfp1/10540335_493883594081307_359212114_n.jpg
Mmoja wa mashuhuda hao, Rajabu Suleiman alisema kuwa moto huo ulianzia katika ghorofa ya msikiti huo, sehemu inayotumiwa na Shule ya Seminari ya Mivumoni Islamic
 “Moto umeteketeza ghorofa ya juu yote yenye shule,” alisema Suleiman.
Alisema askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji walifika katika eneo hilo wakiwa na magari mawili na kuanza kuzima lakini waliishiwa maji na kwenda kufuata mengine.


Shuhuda mwingine, Michael Kopwe alisema akiwa jirani na msikiti huo na wenzake, waliona cheche juu ya msikiti huo lakini walipuuza wakidhani ni michezo ya watoto hadi moto huo ulipolipuka baada ya dakika 15.Akizungumzia tukio hilo, Katibu wa Msikiti huo, Sheikh Abdallah Mohamed alisema moto huo ulianza saa 12:30 jioni na chanzo chake hakijajulikana.
“Tumeshtukia tu moto unawaka na hadi hivi sasa umeshateketeza paa lote la juu, polisi wako hapa pia zimamoto wamekuja lakini wameishiwa maji na moto unaendelea,” alisema Sheikh Mohamed.Sheikh Mohamed alisema ghorofa mbili za juu za msikiti huo ziliteketea na hadi anazungumza na gazeti hili moto ulikuwa unaendelea kuwaka, hivyo kuwa na wasiwasi kuwa huenda hata sehemu ya chini ingeweza kufikiwa.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency