Home » » Jivu la Volkano lawaua watu 30 mlima Ontake.

Jivu la Volkano lawaua watu 30 mlima Ontake.




Takriban wakwea milima 30 huenda wameaga dunia nchini Japan kufuatia kulipuka kwa mlima wa Volcano siku ya Jumamosi na kusababisha kukwama kwa mamia ya raia hao karibu na kilele cha mlima huo
Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha mlima Ontake.

Waokoaji hao wamefanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima huo ambapo ndege ya kijeshi aina ya helikopta ilitumiwa kuwaokoa karibu watu 40 waliokuwa wamejeruhiwa
Zaidi ya wakwea milima 200 walifanikiwa kuteremka kutoka kwa mlima huo wenye urefu wa mita 3000 wakati mlima huo ulipoanza kutupa mawe na majivu bila ya kutoa onyo lolote.
Baadhi yao walisema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency