Home » » Maelfu waendelea kuandamana Hong Kong kushinikiza mabadiliko ya kisiasa

Maelfu waendelea kuandamana Hong Kong kushinikiza mabadiliko ya kisiasa




Maelfu ya waandamanaji huko Hong Kong wamekabiliana na polisi, muda mfupi tu baada ya kiongozi wa serikali katika eneo hilo kutangaza kuaanzisha mazungumzo kuhusu mabadiliko ya kisiasa na uchaguzi katika eneo hilo.

Waandamanaji wanasema wanataka uhuru zaidi wa kisiasa katika eneo hilo na uchaguzi wa huru na haki.

Kiongozi wa eneo hilo Leung Chun-ying hata hivyo hajasema ni lini mazungumzo hayo yataanza ili kuleta mabadiliko hayo yanayoshinikizwa na waandamanaji hao wengi wao vijana.

Waandamanaji hao wamewashtumu polisi kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwasambaratisha, kupita kiasi wakati wa maandamano hayo waliosema ni ya amani.

Mwandamanaji akisaidiwa baada ya kulemewa na mabomu ya kutoa machozi

Waratibu wa maandamano hayo wamekaidi amri hiyo na kuwataka watu wengine zaidi kujitokeza ili kuwaunga mkono katika madai yao ya kuitaka China iwaachie uhuru wa kumchagua kiongozi wao katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017.

Kiongozi wa Mamlaka ya Hong Kong C Y Leung amesema serikali yake imesikiliza na kuzingatia madai ya waandamani lakini inapingana na mpango wao wa kujitenga.

‘’Mimi na serikali yangu tutazingatia sheria za msingi na uamuzi unaostahili wa NPCSC,tutajaribu juhudi zote kutekeleza uchaguzi wa kiongozi mkuu kwa kila anayestahili kupiga kura atafanya hivyo mwaka 2017. Serikali itaanzisha hatua inayofuata ya majadiliano kuboresha katiba hivi hivi karibuni. Inasihi sekta mbalimbali za jamii kushiriki katika majadiliano yenye mantiki kwa Amani na kwa kufuata sheria, kufikia makubaliano na kukubali tofauti pamoja na kuruhusu watu milion tano wenye uhalali wa kupiga kura hapa Hong Kong kumchagua kiongozi mkuu mwaka 2017 mtu mmoja kura moja’' amesema Leung Chung-ying.

‘mimi na serikali yangu tumekuwa wasikivu kwa raia na tumejitolea kudumisha jamii yote. Wananchi wanatakiwa kutoa wanayoyahitaji kwa Amani, mantiki na kisheria, na kuheshimu na kuzingatia mitazamo mbalimbali katika jamii. Serikali ya SAR ya Hongkong imeazimia kupinga utawala usio wa kisheria wa ofisi za serikali kuu au makao makuu ya wilaya ‘utawala wa seriakli kuu’’. Polisi wanajitambua kukabiliana na hali kwa wakati kwakuzingatia sheria’’ Ameongeza
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency