Home » » Kutoka NBA: Timu ya kikapu Pistons yamfukuza Hasheem Thabeet

Kutoka NBA: Timu ya kikapu Pistons yamfukuza Hasheem Thabeet


Timu ya Kikapu ya Pistons imemtema Mchezaji wake kutoka nchini Tanzania, Hasheem Thabeet ambaye amejiunga na Pistons mwezi septemba akitokea klabu ya Philadelphia iliyokuwa imemchukua kutoka Oklahoma City Thunder.

Alicheza dakika tano tu katika mchezo mmoja wa pre season na katika mwezi huu amecheza dakika tano tu dhidi ya Washington Wizard huku akikosa jaribio lake moja na kufunga.

Pamoja na Hasheem Thabeet wengine waliofungasha virago ni Brian Cook, Lorenzo Brown na Josh Bostic.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency