Home » » Msichana anaetumiwa kutukana wagomvi wa mastaa akamatwa.

Msichana anaetumiwa kutukana wagomvi wa mastaa akamatwa.



Mwanadada anyejulikana kwa jina la Maltilda au Maltikibokoyao amaye kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akimkingia kifua mrembo Wema Sepetu kwa kuwatukana mastaa wenye mgogoro na Wema,alitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo chake maalumu cha CyberCrime na kushikiliwa kwa siku nzima kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kituo kikuu cha polisi binti huyo alitiwa mbaloni baada ya kumtukana mtu mmoja aliyekuwa ana ugomvi na wema ambaye aliamua kwenda polisi na kutoa ushahidi kamili amabo ulifanikisha kumnasa baada ya polisi kumuwekea mtego mdogo.

"amekuwa akitukana sana mastaa karibu wote wa Tanzania bila kujali nani ni nani,hadi tunamtia mbaroni alikuwa amewatukana wengi sana,na kwenye simu tulizo mkamata nazo tulikuwa na ushahidi na matusi yake.....Mwazoni alikuwa akijaribu kuficha ukweli aliokuwa nao,lakini baada aya kimweka 'lokapu' kwa siku moja akaeleza msimamo wake"kilisema chanzo

Kesho yake binti huyo aliamua kusema ukweli kuhusu kazi yake ya kutukana watu mitandaoni.na kuwataja mastaa kadhaa wa kitanzania ambao wamekuwa na kawaida ya kuwanunulia simu za kisasa na kuwawekea muda wa maongezi ili wawatukane wenye ugomvi nao,na wote walioshirikiana na maadui zao.

"Aalisema mengi sana na kuwaomba radhi kwa wote alio wai watukana na kuaidi kutorudia tena,ki ukweli huyu binti ameingia mtego wa kuwatukana watu mitandaoni  kwa kuamini kuwa hatojulikana.....Hao wanaojiita mastaawanawatumia hawa  mabinzti kwa ujira mdogo na kujiingiza katika kesi kama hizi kwa ajili ya umaskini wao,"kilisema


Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency