Home » » Vyama visivyokuwa na wawakilishi bungeni vyaungana kupambana na UKAWA.

Vyama visivyokuwa na wawakilishi bungeni vyaungana kupambana na UKAWA.


Wakati vyama vya upinzani vikiwa na umoja wao maarufu kama UKAWA na kutangaza kuungana, vyama visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimetangaza kuungana na kuweka mgombea mmoja kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa lengo likiwa kupambana na UKAWA na Chama Cha Mapinduzi.
Akitangaza jijini Dar es Salaam uamuzi wa kuungana katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakilishi wa vyama Sita visivyokuwa na uwakilishi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha UPDP Bw. Fahmi Dovutwa amesema kuwa wameamua kuungana ili kupambana na UKAWA na CCM ambapo vyama vinavyounda umoja huo ni UMD, SAU, UPDP, AFP, Jahazi Asilia na Demokrasia Makini.
Mmoja wa viongozi wa wanaounda vyama Sita vinavyounda vyama hivyo ambaye ni wenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP) Bw. Rashid Rai amesema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi wa maendeleo hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency