Home » » Diamond ajibu tuhuma ya kuwanyanyasa wasanii wenzake

Diamond ajibu tuhuma ya kuwanyanyasa wasanii wenzake



Hivi karibuni mtandao maarufu hapo Bongo wa kutoa habari za mastaa mbalimbali hapa duniani,ulitoa headline iliyowavutia wengi kuwa Diamond Lawamani Mombasa adaiwa kuwafukuza Nyota ndogo na wasanii wengine vip lounge,atimae aamua kufunguka juu ya tuhuma hiyo.
http://www.bongo5.com/diamond-lawamani-mombasa-adaiwa-kuwafukuza-nyota-ndogo-na-wasanii-wengine-kwenye-vip-lounge-12-2014/

Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila, kwa kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!?? 

Ningependa kutumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki zangu waliokutana na story hizo kuwa sio za kweli ni zenye lengo la kudhoofisha Mahusiano yetu mazuri ya wasanii Wa Africa mashariki..kama BigEye ya Uganda ilivyowahi kuandika habari za upotoshaji Kati yangu na Jose Chameleone.. Pia Nawasihi @Bongofive ni vyema mtambue Nafasi yenu kwenye jamii kwa sasa, Kuweni makini na baadhi ya habari mnazo post ama kureport kutoka baadhi ya mitandao, zinavunja mahusiano mazuri ya wasanii wa East Africa...

kumbukeni kuna watu wana tabia ya kujudge kitu kwa kusoma kichwa cha habari tu pasipo kufuatilia undani wa habari...Yawezakuwa mwaandika kwa nia njema tu, lakini ni vyema muwe mnapata na uhakika kwanza kabla ya kuripoti, hususan story za kutengeneza chuki kama hizi....kufanya hivyo ndiyo mtasaidia kukuza industry yetu ya East Africa...
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency