Home » » Mganga awachoma moto wateja wake wakati wa Tambiko.

Mganga awachoma moto wateja wake wakati wa Tambiko.

 
Mganga wa tiba za asili Omar Kikukwa mwenye miaka 32 Wilayani Kilindi anashikiliwa na polisi kwa kuwachoma moto wateja wake na kusababisha mmoja wao kufariki dunia.
Aziza Hassan mmoja wa wnaafamilia walionusurika katika mkasa huo alisema mama yake pamoja na watoto wake wawili walipelekwa kwa mganga wa kienyeji na baba yao wa kufikia kwa ajili ya kufanyiwa tambiko.

Alisema kuwa walipofika kwa mganga huyo na kuanza kufanyiwa dawa ambapo ilifanyika ndani ya shimo ambalo liliezekwa kwa nyasi juu yake na kuachwa nafasi ndogo kwa ajili ya kuingilia ndani ya shimo waliloambiwa ndipo dawa inatakiwa kufanyika huku baba yao akibaki nje na mganga.

Alisema baada ya muda walidhani mganga ameshamaliza na aliwajibu dawa bado inaendelea na gafla mganga huyo aliwasha moto mkubwa na kuanza kuwaka ndipo akawaamrisha watoke shimoni huku moto ukiendelea kuwaka hadi mlangoni.

Alisema baada ya moto kupungua walitoka huku wenzake wakiwa hawajiwezi kabisaambapo baba yakena mganga waliwakataza kwenda hospitali na kuwaambia kuna daktari wao anakwenda kuwatibu katika kijiji cha jirani na hapo huku mwenzao mmoja akipoteza maisha.

Kwa sasa mganga huyo anashikiliwa na polisi kwa kosa lakusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu kwa moto.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency