Home » » HICHI NDIO ALICHOSEMA MH ZITO JUU YA KURUDI CHADEMA.

HICHI NDIO ALICHOSEMA MH ZITO JUU YA KURUDI CHADEMA.

zito

Mheshimiwa Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini mwanzoni mwa mwaka 2014 alikua na mgogoro mkubwa na Chama chake cha Chadema.Magazeti yaliyotoka siku chache zilizopita yali ripoti taarifa ya Mbunge Zitto Kabwe kurudi tena Chadema,hiki ndicho alichokisema Zitto Kabwe. 
Swali lilikua ni yeye kuhusu kurudi Chadema
'Hapana nadhani hizo ni tetesi kwa sababu sijatoa kauli yoyote kuhusiana na hilo na moja mimi bado mwanachama wa Chadema kwa sababu nina kesi mahakamani na kesi hiyo haijaamuliwa,bado inaendelea’
‘Sijawahi kutoka kwenye uanachama wa Chadema,mtu anaposema nataka kurudi Chadema hayuko sahihi,inafahamika nilikuwa na matatizo na chama hatujaweza kuyatatua,hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika lakini kuna baadhi ya watu wameanza kuleta hayo mazungumzo’.

Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency