Home » » MSIBA CCM:Kifo cha Kapteni Komba kimeacha pengo.

MSIBA CCM:Kifo cha Kapteni Komba kimeacha pengo.



Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) Kapteni John Komba amefariki dunia leo alipokuwa akipelekwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam baada ya kuzidiwa.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Hospitali ya TMJ, ofisi ya Bunge na Chama Cha Mapinduzi na kwamba kwa sasa taratibu za maziko yake zinaendelea kufanywa .

Aidha taarifa za hivi punde kutoka nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach Tangi Bovu zinaeleza kuwa maelfu ya watu kutoka katika kada mbalimbali wanaendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu ili kutoa faraja kwa familia kwani marehemu ameacha mjane mmoja na watoto kumi na moja.

Akizungumza na tovuti hii mmoja wa madaktari aliyempokea wakati anafikishwa hospitali ya TMJ, Dk Elisha Ishan amesema Komba alifikishwa hospitalini hapo saa 10 jioni leo akiwa mahututi .

"Nilimpokea nilianza moja kwa moja kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia," amesema Dk Ishan

Pamoja na hayo Dk Ishan amekwepa kutaja moja kwa moja chanzo cha kifo cha mareheme, hata hivyo amesea Kapteni Komba alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na kwamba siku za karibuni alifika hospitalini hapo kwenye kiliniki yake ya shinikizo la damu.


Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency