Hizi ni baadhi yapicha zinazoonyesha mlolongo mzima wa namna harusa ya Mbunge wa chadema ilivyofana.
Bw Harusi Joshua Nassari akiteremka katika usafiri wake aina ya Range Rover baada ya kufika katika viwanja vya kanisala la Kilinga maarufu kwa Mchungaji Babu.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria ibada hiyo ya ndoa ,Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai katikati.
Bibi Harusi Anande Nnko akiwa amefalia shera lililompendeza.
Wenyeji katika shughuli hiyo akiwemo mzee Samweli Nassari ,baba mzazi wa Jishu wakiwa wanasubili kuulaki ugeni uliokuwa ukiwasili katika kanisa la Kilinga.
Hataimaye Bw Harusi Joshua Nassari akaingia kanisani yeye na wapambe wake na hapa anaye ngojewa ni Bibi Harusi Anande Nko.
Bi Harusi Anande Nko akashuka katika gari alilokuja nalo aina ya Land Cruser VX.
Bwaa Harusi Joshua Nassari akamvisha pete mkewe Anande Nnko.
Bibi Harusi Anande Nnko akamvisha pete mumewe Joshua Nassari
Maharusi wa wakawekewa mikono na Maskofu wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT) David Batenzi.
Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada hiyo (hawapo pichani)
Maharusi wakionesha pete zao za ndoa muda mfupi baada ya kuvishana.
Uthibitsho wa ndoa ni vyeti vya ndoa ,na hapa maharusi wakitia saini katika vyeti vyao.
Wagebi mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ,na hapa ni mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (wa kwanza)
“Mmetuona “ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.
Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo.
Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko.
Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei.
Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani.
Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiwa mbele ya zawadi yao ya Ng’ombe ilitolewa na waumini wa Kanisa la Kilinga ambako ibada ya ndoa ilifanyika,kanisa linaloongozwa na Mchungaji Babu.
Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiteta jambo .
Baba Mzazi wa Joshua Nassari,Mzee Samwel Nassari akimpongeza mwanae kwa hata hiyo.
Mamsapu akianza majukumu ya kuhakikisha Mzee anakuwa nadhifu kila wakati.
Maharusi wakaaga katika viwanja vya Kanisa la Kilenga .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari na ,Anande Nnko wakiwa ndani ya gari muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Kilinga wilayani Arumeru tayari kwa kuelekea viwanja vya Usa-River
Academy.
Msafara ukaanza safari ya kuelekea barabara kuu ya Moshi/Arusha ukitokea kanisani Kilinga.
Baadae maharusi wakabadili gari ili waweze kuonekana vyema na wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki.
Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani.
Kila sehemu msafara wa magari ya maharusi ulipopita ,wakazi wa maeneo hayo walionesha furaha zao .
Barabarani kulijaa na watu walimshangilia Mbunge wao
Bwana harusi na bibi harusi wakionyesha ishara ya chadema.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO