Habari Zetu

Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Inspiration "words"


Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA na yule anayejenga Nyumba ya KAWAIDA.
Anayejenga ghorofa anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza kuinua ghorofa yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka unaweza kukuta yule anayejenga ghorofa bado yuko kwenye msingi. Ila siku akianza kuinua ghorofa lake kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.
Kwenye maisha ndivyo ilivyo - "If want to go so high, you need to go so deep" (Kama unataka kwenda juu sana ni lazima ukubali kwenda chini sana). Ni lazima ufanye kitu cha tofauti kitakochokujengea future imara.
Ukweli ni kuwa Watu wengi wanaokuzunguka wanajenga maisha ambayo ni kama nyumba ya kawaida. Na wewe kama unataka kujenga maisha yanayofanana na ghorofa lazima ukubali kuonekana unachelewa kwenye baadhi ya mambo.
Hii inamaanisha utalazimika kufanya viti vya TOFAUTI na kuwa TAYARI kusubiri. Utatakiwa kuwekeza wakati wengine wanaenda kununua nguo mpya waendane na fashion, utatakiwa kusoma vitabu wakati wengine wanaangalia movie na kupiga stories, utatakiwa uanzishe biashara yako wakati wenzako wamesharidhika na mshahara wanaopata n.k
Unachofanya kuanzia unapoamka hadi unapoenda kulala kitajulisha kama unajenga maisha GHOROFA ama ya KAWAIDA.
Ukijiona unapoteza muda hovyo, ukiingia Facebook/insta ni kusoma umbea tu, unalalamika, unasema utafanya na hakuna unachofanya ujue unajenga maisha ya KAWAIDA tena ni kama nyumba ya UDONGO

Ukitaka kujenga maisha GHOROFA:
Jifunze kitu kipya leo,
Chukua hatua kuelekea Ndoto yako,
Usiwe mtu wa kulalamika bali tafuta suluhisho kwa kila changamoto.

Je,LEO utajiunga na wanaojenga maisha GHOROFA ama wale wanaojenga maisha ya KAWAIDA?

Thanks

Mwenyekiti wa Baraza la maimamu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris auawa kwa risasi.


Mwenyekiti wa baraza la maimam na muhubiri maarufu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa.

Sheikh Mohammed Idris ameuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumbani kwake eneo la Likon baada ya kuvamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha, wakati akitoka nyumbani kuelekea msikitini.

Taarifa kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa Sheikh Mohammed Idris alikuwa akipata vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa kundi la vijana wa kiisilamu wanaodai mabadiliko, na amewahi kutoa taarifa za vitisho hivyo na kusema kuwa anahofia maisha yake.

Decemba mwaka jana Sheikh Idris na mpinzani wake Mohamed Khalifa walinusurika kifo baada ya msikiti wao kuvamiwa na vijana zaidi ya 100, ambao walitawanywa na polisi.

Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya kumbukumbu ya Pandya, mjini Mombasa

Pamekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mauaji ya viongozi maarufu wa dini katika mazingira ya kutatanisha.


Walioitwa katikas usaili serikalini kuanzia june 14 hadi 21 mwaka huu.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/G/25 07 Juni, 2014

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango, Geological Survey of Tanzania (GST) na Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs), anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanywa kabla ya usaili kuanza.
2. Usaili wa ana kwa ana utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Wafike na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Wafike na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8. Kila msailiwa azingatie muda, tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
12. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa kwenye tangazo.

Baada ya kufulia:Mabaunsa wamshusha Chid benz stegini New maisha club Dodoma.




Chini benz Jana Jumapili wakati anafanya show New maisha Club Dodoma alifanya kitendo ambacho baadhi ya mashabiki walimwona kweli jamaa sasa ameshaanza kuwa chizi.


wakati akiwa anafanya Show Katikati ya baada ya mzuka kumpanda Chid alichafua hali ya hewa baada ya kuzama mfukoni na kutoka Bonge la kipisi cha Bangi kilichoshiba na kukiwasha pale pale jukwaani bila hata Uwoga... Hapo ndipo Baunsa wa Maisha kabla akambadilikia kama Mbogo na kumpora hiyo bangi ili asiendelee kuivuta. Kitendo hicho cha kuvuta bangi Club kimeshushia heshima Msanii huyo ambaye ni kioo cha Jamii


Hapo Chidi Benz akiwa kashikiwa bangi na Shabiki wake na kutoa kibiriti cha gesina kuiwasha kama unavyoona hapo



hapo akiwa anavuta Bangi bila ya uwoga... Pembeni ni Baunsa akimwomba akiustaarabu asivute bangi hiyo lakini chid akawa hajili na kuendelea kufanya yake.

   Chanzo:BossngasaTanzania


Tuwache michina:Miti shamba inayofanya matiti kuwa makubwa na yaliyosimama




MATITI ya mwanamke kuwa katika shepu bomba ni shauri la wanawake wengi na si shauri la mtu mmoja tu. Aidha ni sehemu ya mwili wa mwanamke inayotoa msisimko mkubwa.
Wapo wanawake ambao wana musuli nyingi za matiti na hivyo wanakuwa na matiti makubwa na wengine wana kiasi kidogo na hivyo kuwa na matiti madogo.
Hali hiyo ina sababu zake ingawa wataalamu wanasema kwamba ukubwa wa maziwa huambatana na historia ya familia, umri,kupungua kwa uzito, ujauzito unene na kunyumbuka kwa ngozi ya kwenye matiti, kiwango cha homoni hasa estrogen na progesterone.
kwa kuwa matiti ya mwanamke ni sehemu ya utambuzi wake wa ukike na mwenyewe alivyo na pia ni alama ya uzazi na salama kwa mtoto wake.
Uzuri wa matiti ni kuwa mazima na kama kukitokea kasoro kidogo tu huwa ni kasheshe kubwa kwa upande wa mwanamke. Kutokana na hili nashauri wanawake kuwa na tabia ya kutunza matiti yao ikiwa ni pamoja na kuyakagua na kama kuna kasoro kuyafikisha kwa wahusika kuangalia tatizo.
Usafi wa mwili huambatana na kuyatunza vyema matiti yako.
Lakini wengi wanaotaka matiti makubwa ndio ho wanaopata adhabu ya kusaka matiti hayo kwa udi na uvumba.
Uzuri wa matiti
zipo njia nyingi za kuwa na matiti bomba na kwa sasa duniani matiti bomba ni yale makubwa( nadhani hii ni fasheni).Unaweza kupata matiti hayo kwa upasuaji au na kwa kupachika kitu ndani hasa silikoni na nyingine ni kutumia dawa ambapo misuli hujazia na kuyafanya matiti kuwa makubwa.
Njia ya kukuza matiti kwa salama ni kutumia dawa ambazo zimetolewa katika miti shamba, mitishamba ambayo ikichanganywa pamoja inafanyakazi mbalimbali ya kuboresha ukubwa na uimara wa matiti.
Mitishamba hii inatoka sehemu mbalimbali na Afrika Kusini wamefanikiwa kutengeneza dawa kutokana na miti hii na wanaotaka urembo wa matiti makubwa na yenye kuonekana wanapata nafasi kubwa ya kununua dawa hiyo.
Aidha baada ya kujazia matiti yako na kuwa makubwa kitu kinachofuata ni kuhakikisha kwamba matiti yako hayalegei na kuwa katika ukubwa wake bado yanasimama katika saa inayotakiwa na yenye raha yake si kutazama bali pia kuyatomasa.
Matiti hupendeza zaidi baada ya kuonekana yakiwa yametulia na yanayokubali brasia zenye maana duniani.
Aidha uzuri mwingine utatokana na kuwezesha matiti yako imara kwa kufanyia hali ya kuwezesha musuli za maziwa kufanyakazi yake.
Pamoja na kuongeza ukubwa wa matiti ni vyema kama ngozi yako inakuwa na rangi ile inayofaa huku ukihakikisha kwamba chini ya maziwa jacho halikai na wala brasia haisababishi wewe kuwa na kazi ya ziada katika usafi wa eneo hilo.
Ipo haja ya kutumia mafuta yanayostahili kukata mnururisho mkali wa mwanga unaoweza kusababisha kansa ya ngozi.
Kliniki moja ya Afrika Kusini St Herb Beauty Breast Care imetengeneza aina fulani ya mitishamba yenye mchanganyiko maridhawa kwa ajili ya matumizi ya wanawake wanaotaka urembo wa matiti makubwa na yaliyosimama bila upasuaji wala kutumbukiza kitu katika matiti hayo.
Ni lazima kuwe na mizania ya mitishamba kupata kile kitu unachotaka. Kliniki hiyo imekuja na fomula yake inayoitwa Beauty Bust Herbal Breast Enlargement Formula ambayo hushawishi kukua kwa misuli za matiti bila kushawishi uzalishaji wa maziwa na kuyaongezea uzuri matiti yako.
Pamoja na matiti hayo kuwa bora kwa matumizi hayo, matiti makubwa hulainika sana unapokuwa mzee na hili ndilo hasa nililotaka kusema, mazoezi ya mwili husaidia sana bado kuweka matiti katika shepu yake.
Kama u kijana na matiti yako yanakuwa malapa basi huenda tatizo si tu musuli zimelegea bali pia huvai brasia kukusaidia. maziwa yanaweza kuwa malapa kwa kutokuwa na kitu cha kusaidia kusimama.Hili ni wazi zaidi kwa wanawake wenye matiti makubwa au watu ambao wanafanya mazoezi bila kuwa na sapoti ya brasia.Pia matiti yanaweza kuwa malapa kutokana na kujifungua
Lakini ukitaka uhakika wa uzuri wako kwa namna ya kuwa na matiti makubwa na yalioyosimama vyema ni lazima utumie dawa hizi za matishamba ambapo mchanganyiko wake ndio umetoa fomula ya St Herb :
Fenugreek :
Kwa kawaida matunda ya mmea huu yalikuwa yanatumika na wanawake wa Kigiriki kuongeza ukubwa wa matiti yao na imehakikishwa kisayansi kuwa mtishamba huu huongeza athira ya mastogenic kwa misuli inayotengeneza maziwa.
matunda( mbegu ) ya mtuii huo yalikuwa yanatengeneza aina ya dawa ijulikanayo kama phytochemical diosgenin na estrogenic isoflavones zinazooongeza utengenezaji wa dawa ya estrogen katika mwili, dawa ambayo ni ufunguo kwa matiti yenye shepu ya mchonoko na yaliyojaa.
Mmea wa Saw Palmetto:Huu ni mmea wa kaskazini mwa Marekani na kwamba unafanana na mtende ni moja ya mmea wenye kemikali chache unaotengeneza musuli na husawazisha matatizo ya mkaziwa yenyewe.
Fennel Seed:Husaidia kuzalisha musuli nyingine mpya
L-Tyrosine:Hii ni amino acid, Tyrosine ambayo hudhibiti uzalishaji wa homoni na hivyo kupunguza unene na.
Mexican Wild Yam:Matumizi ya kila siku yanapunguza michirizi isiyotakiwa katika matiti.
Kelp:Ni zao la baharini. Ni chanzo bora cha madini ya iodine chakula chenye hiki huleta homoni zilizojipanga vyema.
Damiana:Kikawaida hutumika kwa ajili ya kuleta mizania ya homoni.Kuleta ukuzi mwema wa matiti, kupunguza dalili za matatizo yanayoambatana na siku za hedhi na kuchanganya ashiki;husaidia kupunguza uzito kuleta nguvu na kuondoa uchovu.
Dong Quai:kikawaida mmea huu wa Asia hutumika kuripea seli ikiwemo ya mammorianna, (tezi za matiti).
Mother's Wort:Mmea uliopo sehemu nyingi za Ulaya na kandoni mwa mito ambazo hutoa msukumo fulani katika kano la uzazi.
Black Cohosh :Mmea unaopatikana kaskazini mwa Marekani hutumika kama dawa ya kubadilisha homoni.
Avena Sativa:Ni kama shayiri na ina kiasi kikubwa cha saponins, flavonoids, minerals, na alkaloids kwa ajili ya mfumo wa homoni.
Humulus Lupulus:Husaidia kuimarisha matiti.
kisasili cha matiti
1. Kujiamini kwa mwanamke kumejikita zaidi katika ukubwa wa matiti yake
2. Wanawake hawana muwashawasha sana na ukubwa wamatiti yao
3. Brazia za kimichezo si za lazima.
4. matiti makubwa yanauhusiano na mambo ya ngono
5. Wanawake na matiti madogo hushindwa kunyonyesha kwa ufanisi
6. Wanawake wote hufurahia kutomaswatomaswa kwa matiti yao
7. Wanawake kwa kawaida huwa na matiti mawili yenye ukubwa unaofanana
8. Nywele kuzunguka chuchu huonyesha kwamba mwanamke huyu si wa kawaida
9. Wanawake na matiti makubwa ni wazazi sana
10.Unyonyeshaji husababisha matiti kuwa malapa

Show ya Jahazi modern Taarabu kizungumkuti.



Show ya Jahazi ambayo ilikuwa ifanyike leo ukumbe wa Travertine hotel hatimie show iyo haitafanyika tena kutokana na kutokea kwa msiba unaemuhusisha mmiliki wa hotel hiyo kufiwa na rafiki yake wa karibu ambae pia alikuwa ni sehemu ya watendaji katika hotel hiyo.

Aidha pia inasemekana kuwa leo ndio siku ambayo wapenzi wa bendi hiyo walikuwa wakiisubiria  kwa hamu,kwani ni show ya kwanza kwa wilaya ya Kinondon ndani ya Dar tangu wiki tatu zilizopita walipoondoka kwa ziara ya mikoani.

Mzimu wa mauti kuwatafuna Bongo movie:Mzee Small aaga dunia.



Baada ya uvumi mkubwa kuenea ndani ya mitandao mikubwa ya kijamii kuhusu kifo cha muigizaji mkongwe wa vichekesho Mzee Small tangu usiku wa saa sita,sintafahamu hizo zimetatuliwa kwa majonzi makubwa.

Awali majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo habari zilienea kote kuwa Mzee Small amefariki akiwa katika hospital ya Mwananyamala jambo ambalo halikuwa sahii.

Mzee Small kama jina la umaarufu wake huku jina lake kamili ni Said Ngamba amefariki usikuwa leo akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar iliyopo Upanga . 
Imedhibitishwa Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa Presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka . 
Mtoto wa marehemu Muhidin amethibitisha rasmi juu ya kifo cha Said Ngamba (Mzee Small).
Mungu ailaze roho yake mahari pazuri.

Mume wa Frola Mbasha afunguka na kukiri.

Kutokana na sakata la kesi ya mume wa Frola Mbasha kumbaka shemeji yake na kufuruga penzi nzima na mwanamziki mwa injili.
Hii ndio audio analiyoamua kufunguka na kueleza kinagaubaga chote.

Aibu tupu:Flora Mbaya anamkosi wa wadogo zake.

  
Baada ya kuvunjika kwa ndoa iliyo dumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ilikubwa na visa vingi ,haya ndio Mbasha aliwahi sema toka katika chanzo kimoja cha habari.
                       “Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi,Flora naye alikuwa na nyendo zake mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka kwenda gym (sehemu ya mazoezi) anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu ya ndugu wa mke ikawa kubwa kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo yalipofikia pabaya kabisa.”

Hivi karibuni imeenea tuhumu kubwa hasa katika mitandano ya kijamii kuhusu mume wa Frola Mbasha kumbaka mdogo wa Frola Mbasha  pichani.
Mdogo wake Flora anaedaiwa kutembea na Mr Mbasha
Kuhusu ugomvi huo, hivi karibuni Flora alikaririwa katika vyombo vya habari akisema hana tatizo na mumewe na ameshasamehe na kusahau yote yaliyopita hivyo ajitokeze tu ili akajibu mashitaka ya kudaiwa kubaka binti wa miaka 17 yaliyofunguliwa.
“Mimi sina tatizo kabisa na mume wangu, nimeshasamehe yote yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza kuyafuta kama ningekuwa mimi ndiye niliyemshitaki,” alisema Flora.

Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika Kituo cha Polisi cha Tabata Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha.

Aidha imekuwa sio jambo geni kwa wadogo wa Flora Mbasha kuhusiswa katika maisha ya kumtia ainu na kumchafulia heshima yake ndani ya jamii.

Kumbuka pia ile movie ya picha chafu iliyotoka inayomuhusu Mrisho Ngasa na binti aliyedaiwa pia ni mdogo wa Frola Mbaya.


Kutokana na mvutano huo pamoja na kesi hiyo ya kudaiwa kubaka inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila mmoja hana imani na mwenzake tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama zamani linakuwa gumu kuliko ngamia kupenya kwenye  tundu la sindano.

HIZI NDIO PICHA ZA HARUSI YA MBUNGE WA CHADEMA ,BWANA JOSHUA NASSARI NA BI ANANDE NNKO



Hizi ni baadhi yapicha zinazoonyesha mlolongo mzima wa namna harusa ya Mbunge wa chadema ilivyofana.



Bw Harusi Joshua Nassari akiteremka katika usafiri wake aina ya Range Rover baada ya kufika katika viwanja vya kanisala la Kilinga maarufu  kwa Mchungaji Babu.



Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria ibada hiyo ya ndoa  ,Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai katikati.


Bibi Harusi Anande Nnko akiwa amefalia shera lililompendeza.


Wenyeji katika shughuli hiyo akiwemo mzee Samweli Nassari ,baba mzazi wa Jishu wakiwa wanasubili kuulaki  ugeni uliokuwa ukiwasili katika kanisa la Kilinga.


Hataimaye Bw Harusi Joshua Nassari akaingia kanisani yeye na wapambe wake na hapa anaye ngojewa ni Bibi Harusi Anande Nko.



Bi Harusi Anande Nko akashuka katika gari alilokuja nalo aina ya Land Cruser VX.


Bwaa Harusi Joshua Nassari akamvisha pete mkewe Anande Nnko.


Bibi Harusi Anande Nnko akamvisha pete mumewe Joshua Nassari




Maharusi wa wakawekewa mikono na Maskofu wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT) David Batenzi.


Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada hiyo (hawapo pichani)


Maharusi wakionesha pete zao za ndoa muda mfupi baada ya kuvishana.



Uthibitsho wa ndoa ni vyeti vya ndoa ,na hapa maharusi wakitia saini katika vyeti vyao.


Wagebi mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ,na hapa ni mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (wa kwanza)


“Mmetuona “ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.


Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo.


Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko.



Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei.



Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani.



Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiwa mbele ya zawadi yao ya Ng’ombe ilitolewa na waumini wa Kanisa la Kilinga ambako ibada ya ndoa ilifanyika,kanisa linaloongozwa na Mchungaji Babu.


Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiteta jambo .


Baba Mzazi wa Joshua Nassari,Mzee Samwel Nassari akimpongeza mwanae kwa hata hiyo.


Mamsapu akianza majukumu ya kuhakikisha Mzee anakuwa nadhifu kila wakati.


Maharusi wakaaga katika viwanja vya Kanisa la Kilenga .


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari na ,Anande Nnko wakiwa ndani ya gari muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Kilinga wilayani Arumeru tayari kwa kuelekea viwanja vya Usa-River
Academy.



Msafara ukaanza safari ya kuelekea barabara kuu ya Moshi/Arusha ukitokea kanisani Kilinga.


Baadae maharusi wakabadili gari ili waweze kuonekana vyema na wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki.





Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani.





Kila sehemu msafara wa magari ya maharusi ulipopita ,wakazi wa maeneo hayo walionesha furaha zao .
Barabarani kulijaa na watu walimshangilia Mbunge wao


Bwana harusi na bibi  harusi wakionyesha ishara ya chadema.

 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency