Home » » Matumizi ya Mayai kwa urembo wako wa Ngozi na Nywele.

Matumizi ya Mayai kwa urembo wako wa Ngozi na Nywele.



YAI limekuwa na matumizi kama chakula kwa muda mrefu, wapo ambao hutumia chakula hicho kwa kukaanga, kuchemsha, kunywa likiwa bichi na au kuchanganya katika vyakula vingine mbalimbali.Lakini pia kuna matumizi ya Yai zaidi ya chakula, kwani linauwezo mkubwa wa kurutubisha ngozi,  nywele na pia kuondoa uchovu.
Jinsi ya kufanya ukitaka kutumia Yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako.
Chukua Yai, changanya na asali kijiko kimoja cha chai  mafuta ya Olive .Chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni, kaa nao kwa dakika kumi hadi 15. Hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi kubana.
Pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua, mafuta au krimu usoni.Unaweza kutenganisha kiini cha Yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya  hapo pigapiga ule ute  hadi uwe na mapovu kisha chukua povu,  linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke .
 Baada ya hapo osha na maji ya uvuguvugu, ukifanya hivyo mara kwa mara itakusaidia kufanya ngozi yako iwe anga’avu.Kama umetoka kazini na unaonekana umechoka na unataka kutoka usiku, chukua ute wa yai na pakaa chini ya jicho na uache kwa dakika 10 hadi 15 kisha safisha, itasaidia kuondoa muonekano wa uchovu katika macho yako.
Iwapo unasumbuliwa na kuwashwa ngozi, matumizi ya Yai pia ni njia sahihi kuepuka tatizo. Maski ya Yai ina utajiri wa ‘Acid’ za Amino ambazo husaidia kupunguza na kuondoa miunguzo au muwasho mwilini kutokana na protini inayopatikana kwenye Yai.
Kama unawashwa mwili mzima,  chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea ndani ya siku chache utaona matokeo.

Kwa upande wa nywele wale ambao, nywele zao hazina afya au ukuaji wao ni hafifu wanaweza kupaka yai kichwani, hakikisha inagusa  mizizi inayosaidia kuotesha nywele, kama nilivyoeleza awali protini iliyopo kwenye yai ndio chanzo cha kila kitu.Unaweza kutumia Yai kama ‘Hair Conditioner’, chukua kiini chake changanya  na asali, mafuta ya watoto na maji kidogo.
Changanya  vizuri kisha paka kichwa kizima acha kwa dakika 20 kisha osha na maji ya baridi chukua ute mweupe changanya  na shampoo yako kidogo
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency