Baada ya uvumi mkubwa kuenea ndani ya mitandao mikubwa ya kijamii kuhusu kifo cha muigizaji mkongwe wa vichekesho Mzee Small tangu usiku wa saa sita,sintafahamu hizo zimetatuliwa kwa majonzi makubwa.
Awali majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo habari zilienea kote kuwa Mzee Small amefariki akiwa katika hospital ya Mwananyamala jambo ambalo halikuwa sahii.
Mzee Small kama jina la umaarufu wake huku jina lake kamili ni Said Ngamba amefariki usikuwa leo akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar iliyopo Upanga .
Imedhibitishwa Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa Presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka .
Mtoto wa marehemu Muhidin amethibitisha rasmi juu ya kifo cha Said Ngamba (Mzee Small).
Mungu ailaze roho yake mahari pazuri.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO