JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/G/25 07 Juni, 2014TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango, Geological Survey of Tanzania (GST) na Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs), anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanywa kabla ya usaili kuanza.
2. Usaili wa ana kwa ana utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Wafike na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Wafike na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8. Kila msailiwa azingatie muda, tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
12. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa kwenye tangazo.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO