Home » » Madhara ya Uzito Mkubwa

Madhara ya Uzito Mkubwa

KILA siku tunazungumzia masuala ya kuweka ngozi safi na sura bomba lakini mara zote huwa tunasahau kuzungumzia uzito ambao ama hakika ni kitu kibaya kuliko kitu chochote kile. Uzito ni sawa na uvutaji wa sigara ambao huleta matatizo makubwa kwa watu ambao wamo katika kilinge hicho. wataalamu wa afya na urembo wanasema wazi kuwa kuwa mnene kunapunguza siku namna ya kujiweka sawa katika masuala mbalimbali ya kijamii lakini pia unakuwa na muda mfupi sana wa kuishi duniani. Wataalamu wanasema kwamba kuwa mzito kunapunguza maisha yako kwa miaka mitatu na haya yamesemwa na mtafiti Gary Whitlock kutoka Clinical Trial Service Unit ya chuo kikuu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza. Uzito huu ni ule unaokuwa mara tatu ya uzito ambao unatakiwa mtu awe nao kutokana na urefu wake,umri na pia afya yake. Ndio kusema kama mtu anakuwa na uzito mathalani paundi 150, mtu huyu anapunguza umir wake wa kuishi hapa duniani kwa miaka 10. Kwa maelezo mengine uzito wa aina hii ni sawa na uvutaji wa sigareti ambapo pamoja na kuchakaza ngozi pia hupunguza maisha ya mtu kwa miaka kumi. Ndio kusema katika urembo pamoja na kupiga vita sigareti uzito wa kuchusha nao lazima upigwe vita.           
                                            Kwa  waafrika kuwa mnene ni bomba, pamoja na ukweli wa kiutamadunikwamba kuwa mnene ni kutamu kwani unakuwa na nyama za kushikwa lakini ni vyema watu wakatambua kwamba uzito wa kuchusha yaani mara tatu ya ule unaostahili kuwa nao ni hatari kubwa kwa maisha yako. Onyo hili la wataalamu limefanywa baada ya uchunguzi kwa watu 894,576 waume kwa wake katika tafiti 57 zilizofanywa. ingawa tafiti hizi zilifanywa kwa watu wa Kaskazini mwa Marekani na Ulaya kwa watu wenye ujazo wa 25 (BMI) hata hapa nchini watu wanastahili kuangalia suala la uzito wao. Kwa taarifa yako uzito wa kuchusha huleta tatizo la figo, ini na aina kadha za kansa na pia hyuleta matatizo ya magonjwa ya moyo na kiharusi. Unene huleta mchosho mkubwa kwa moyo na pia kuleta mizania dhaifu ya rehemu na kusababisha shida katika mwenendo wa damu. Wanaume wenye kiuno kikubwa huongeza hatihati ya kifo wakatiw nawake wenye mzunguko mkubwa huongeza hati hati ya kifo kwa asiulimia 78.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency