Home » » Njia Rahisi ya kupunguza tumbo

Njia Rahisi ya kupunguza tumbo

                                Wengi wa wasomaji wamemtumia meseji za kutaka kujua njia ya kupunguza mafuta tumboni, wanawake kwa wanaume walituma maswali kwa wingi. Njia iliyosalama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kupunguza tumbo kubwa ni ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.
Nilipata nafasi wiki hii ya kuzungumza na daktari mmoja katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambaye sitamtaja kwa jina na alikuwa na mengi ya kuelezea jinsi hali hiyo inavyoanza na husababishwa ni nani. Alisema kuwa,kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi. Vyakula kama viazi mviringo, wali mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu inasababisha kuongezeka uzito na pia huongeza ukubwa wa tumbo,vyakulahivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi kidogo sana. "Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko kawaida hali hiyo inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi, kutokunywa maji ya kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum" anasema. Anasema kuwa kama ntu anataka kupunguza mafuta au kuondoa kitambi anatakuwa kula milo mitatu kwa siku na si kujinyima kula kwa kudhani kuwa unaweza kupungua uzito. "Vyakula vya wanga na mafuta ufanya mtu kunenepa, acha au kupunza kula vyakula vyenye wanga ili kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini, mafuta yanaporundikana mwilini athari moja kubwa ni kuwa na tumbo kubwa." anasema. Anasema kuwa,tumbo kuwa kubwa ni dhahiri kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya mwili. "Kwa kuwa Chakula hiki cha ziada huwa hakitakiwi, mwili hukibadilisha na kuweka akiba katika mfumo wa mafuta kitaalamu kama glycogem.Unaweza kukabiliana na kuzidi kwa protini zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba kwa mfumo huo wa mafuta" Daktari huyo anasema kuwa, mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia mlo wake kwa siku.
"Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika hali inayotakiwa. "Watu wengi wanatumia wanga mwingi wakati wa usiku muda ambao unaenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa tumboni" anasema Daktari. Je Mazoezi husaidia kupunguza uzito wa mwili na manyama uzembe? Mazoezi ya viungo yamethibitishwa kusaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili. Kutokana na hali ya ulaji unaweza kutengeneza manyama uzembe katika kifua, mapaja na maeneo fulani ya tumbo ambayo yametengenezwa kupokea maeneo ya ziada yanayotokana na mafuta yenyewe au sukari iliyobadilishwa kuwa mafuta. Nishati inayotokana na nafaka ambayop haiwezi kutumika muda huo hutengenezwa kuwa mafuta na kupelekwa eneo husika. Wanaume huwa na asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na ni kawaida wakati kwa wanawake ni asilinia 13 hadi 25.
Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili. Mafuta yanayounguzwa kwanza ni yale ya kawaida kabla ya kuingia katika akiba. Kuna umuhimu wa kutambua kuwa mazoezi ni kitu cha bure na kama ukifanya kwa mpangilio na vizuri hutakuwa na shida ya kutengeneza shepu yako. Dk.Martica Heaner,M.A, M.Ed. ambaye hutoa mawaidha ya keep fit ndani ya MSN anasema ni jambo la heri kama mtu atakula kidogo kabla ya kuanza mazoezi ili kutoa nishati ya kutosha ya kufanyisha mazoezi. "Lakini kama unaenda mwendo fulani mdogo tu au unatembea kwa dakika 30 huenda usiwe na haja kabisa ya kula hata hicho kidogo na hasa ikiwa uliweka kitu kiogo saa tatu zilizopita" anasema.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency