Habari Zetu

Showing posts with label Tips. Show all posts
Showing posts with label Tips. Show all posts

Inspiration "words"


Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA na yule anayejenga Nyumba ya KAWAIDA.
Anayejenga ghorofa anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza kuinua ghorofa yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka unaweza kukuta yule anayejenga ghorofa bado yuko kwenye msingi. Ila siku akianza kuinua ghorofa lake kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.
Kwenye maisha ndivyo ilivyo - "If want to go so high, you need to go so deep" (Kama unataka kwenda juu sana ni lazima ukubali kwenda chini sana). Ni lazima ufanye kitu cha tofauti kitakochokujengea future imara.
Ukweli ni kuwa Watu wengi wanaokuzunguka wanajenga maisha ambayo ni kama nyumba ya kawaida. Na wewe kama unataka kujenga maisha yanayofanana na ghorofa lazima ukubali kuonekana unachelewa kwenye baadhi ya mambo.
Hii inamaanisha utalazimika kufanya viti vya TOFAUTI na kuwa TAYARI kusubiri. Utatakiwa kuwekeza wakati wengine wanaenda kununua nguo mpya waendane na fashion, utatakiwa kusoma vitabu wakati wengine wanaangalia movie na kupiga stories, utatakiwa uanzishe biashara yako wakati wenzako wamesharidhika na mshahara wanaopata n.k
Unachofanya kuanzia unapoamka hadi unapoenda kulala kitajulisha kama unajenga maisha GHOROFA ama ya KAWAIDA.
Ukijiona unapoteza muda hovyo, ukiingia Facebook/insta ni kusoma umbea tu, unalalamika, unasema utafanya na hakuna unachofanya ujue unajenga maisha ya KAWAIDA tena ni kama nyumba ya UDONGO

Ukitaka kujenga maisha GHOROFA:
Jifunze kitu kipya leo,
Chukua hatua kuelekea Ndoto yako,
Usiwe mtu wa kulalamika bali tafuta suluhisho kwa kila changamoto.

Je,LEO utajiunga na wanaojenga maisha GHOROFA ama wale wanaojenga maisha ya KAWAIDA?

Thanks

UMUHIMU WA MATANGO



WATAALAMU wamesema kwamba matango ni chakula muhimu sana katika mwili wako kutokana na kufanhyakazi mbalimbali za kuuweka sawa pamoja na kuupa maji.
Ni vyema kuhakikisha kwamba kila siku unakula tango kwa afya yako.
Hakika kama upo bize sana kiasi cha kusahau kuinywa maji ya kutosha, kula tango ambalo asilimia 90 ni maji. tango litakuongezea maji unayohitaji.
Tango pia linakabiliana na joto nje na ndani ya mwili. ndio kusema kwa kula tango mwili unapunguza mashambulio ya kiungulia. Pia kama utajipaka tango utapata nafuu sana dhidi ya miale ya jua.
Kazi nyingine ya tango ni kupunguza sumu katika mwili, maji yote yaliyomo ndani ya tango linafanya liwe kama fagio la kuondoa sumu mbalimbali mwilini na ulaji wa kila mara wa tangu unasaidia kuondoa mawe katika figo (kidney stones).
Aidha tango linasaidia kukupatia vitamin.Tango lina vitamin nyingi zinazohitajika katika mwili kwa siku. Kuna vitamin A,B,C ambazo hupiga busti katika mfumo wako wa kinga kukupa uangavu na nishati unayoihitaji.
unaweza kufanya jusi ya tango kuwa na nguvu zaidi kw akuichanganya na karoti na spinachi.Usimenye tango lioshe na kulila na unaposaga kupata juisi vivyo hivyo kwani ngozi yake inavitamini C kiasi cha asilimia 123 ya inayohitajika kila siku katika mwili.

UTUNZAJI WA LIPS


Hakuna raha kama kuwa na midomo (lips) zenye kuvutia tena ikiwa katika namna ambayo kila moja anaitamani kuiangalia na hata kuibusu. 
Lips nzuri zina nafasi yake katika maisha ya mwanamke kwani anakuwa mwenye kujiamini tofauti na mtu ambaye anakuwa na midomo mikabu ambayo imekuwa ikipasuka mara kwa mara.
Kuna njia nyingi za kutunza Lips ikiwemo zile za kiasili na hata za kisasa lakini yote hayo hutegemea na matakwa na hata uwezo wa mhusika.
Kumekuwa na hali mbalimbali ambazo hupelekea midomo kuwa mikavu, kukatika na hata kuchubuka na kuwa na ngozi nyekundu.
Kinachoonekana zaidi ni kuwa watu wengi hawatilii sana maanani juu ya utunzaji wa midomo licha ya kuwa kuna wakati midomo inakauka au kupasuka pasuka hasa wakati wa baridi.
Midomo imekuwa ikitunzwa kwa njia za asili ikiwemo kupaka Glycerin hali inayochangia kulainisha ngozi za mdomo na kujiepusha na mipasuko.
Njia hii ya kupaka mafuta hutumiwa wakati wote hata pale mtu anapotaka kwenda kulala.
Pia mafuta haya husaidia kuondoa weusi uliopo kwenye midomo.
Pamoja na hayo pia kuna mafuta maalum ambayo hutumiwa kwa ajili ya kupaka mdomoni kwa lengo la kulainisha midomo ambayo pia kwa kiasi kikubwa inachangia wengi kuwa na midomo inayovutia hasa kwa wale wanaotumia.
Aidha kuna njia ya kutumia majani ya hiliki ambapo hutumika kwa  kusugua kwenye midomo na kupelekea midomo kuwa laoini.
Jambo lingine linalosisitizwa katika utunzaji midomo ni pamoja na kutumia maji ya limao yaliyochanganywa na asali kwa kupakwa kwenye midomo na kukaa na mchanganyiko huo kwa muda wa saa moja hiyo husaidia pia kuondoa hata weuzi uliopo kwenye midomo.
Pia Unywaji wa maji mengi husaidia katika kuimarisha midomo na hata matumizi ya mlozi (almond oil) kama yakipakwa mdomoni kabla ya kwenda kulala husaidia sana kuiweka midomo katika namna inayopendeza.

MAVAZI YANAVYOATHIRI MUONEKANO WA MTU.




Muhimu kutambua mavazi ni njia kubwa na nzuri ya kutambulisha tabia ya Mtu. Wengi wanapendwa au wanachukiwa kutokana na mavazi wanayovaa. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na heshima ama kwa kuwa mafupi au yamekuwa yakiacha sehemu kubwa ya kifua kuwa wazi.
Wasichana wa sasa wanaona kuvaa nguo zinazoacha wazi sehemu kubwa ya matiti kama fasheni.
Kuna mavazi ya aina nyingi ambapo yakivaliwa humfanya mtu apendeze au achukize. Uvaaji wa nguo unatakiwa kuzingatia umri na rangi ya mwili na pia mazingira ya nguo inapovaliwa.
Sio kila nguo ni ya kuvaliwa mchana na sio kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina nyingine za nguo hazistahili kuvaliwa barabarani unapotoka tu barabarani unaanza kupigiwa miluzi hiyo si sawa sawa.
Mathalani wewe ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaaje, kujiweka mrembo na mtanashati ni kitu muhimu. Siku hizi kuna mitimbo mbalimbali ya nguo za madukani, kushona mitindo ya kutumia vitenge, vitambaa kwa mitindo ambayo inatunza heshima ya mvaaji.
Unatakiwa kuvaa kulingana na mahali na wakati kwani kuna nguo za kazini na za kutokea lakini sasa hivi si ajabu ukakutana na mtu mchana wa jua kali akiwa amevaa nguo ya usiku au kumkuta akiwa amevaa viatu virefu huku akijua fika anatembea kwa miguu kwa umbali mrefu.

ATHARI YA NGOZI KUUNGUA NA JUA




Kuna  Msomaji ametuma swali akisema kuwa, yeye ni mwaume mwenye umri wa miaka 30 na amekuwa akifanya shughuli zake chini ya mti ambapo licha ya kuwa na jua kali wakati mwingine kunakuwa na upepo mkali, hali hiyo imesababisha ngozi yake kuungua na jua na ngozi yake kukakamaa imekuwa na makunyanzi kiasi cha kumtisha.
Kulingana na tafiti mbalimbali za kiafya, watalaam wanasema kuungua na jua usoni kunalazimisha ngozi kuongeza uzalishaji wa melanin hali ambayo husababisha mtu kuwa na ngozi nyeusi na kuwa kama kahawia (brown).
Pia unaweza kupata ngozi nyeusi au kahawia kama miale ya jua inakuwa inakupiga moja kwa moja usoni kwa asilimia 60 hadi 80.
Vitamin E inaonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia mtu asipigwe na  miale ya jua usoni, vitamin E hupatikana  katika vyakula kama mafuta ya soya, karanga, nafaka, mboga za majani, kini cha yai na nafaka ambazo hazijakobolewa.
Vitamini E husaidia kukua kwa nywele mara mbili ya kiwango cha ukuaji wa kawaida, pia matumizi ya lotion za kuzuia kuungua na jua zinasaidia sana ili kujikinga na miale ya jua.
Aidha kuungua na jua huwapata  watu ambao mara nyingi hufanya kazi zao wakiwa juani  aina nyingine ya ngozi  ni rahisi sana kuathiriwa na jua na zinahitaji ulinzi zaidi.
Pia ni vizuri kama kila moja atachukua tahadhari mapema ili kujilinda na kulinda ngozi yake isipate tatizo hili.
Watu ambao ngozi zao zimeathirika na jua wanatakiwa kuepuka kushinda juani na wanatkiwa kunywa maji mengi na kula mboga za majani na matunda kwa wingi ili kuweza kurekebisha tatizo lililopo.
Kwa wale wenye makunyanzi kabla ya umri wanashauriwa kula vyakula vyenye chumvi au sukari kiasi kwani matumizi makubwa ya sukari na chumvi ni chanzo cha kuwa na makunyanzi.
Ikumbukwe kuwa kuna vuitu vingi ambavyo miili yetu inahitaji ili kuwa na ngozi nzuri kana usingizi wa kutosha, kupumzika, kufanya mazoezi na kula vizuri.

UTUNZAJI WA MIKONO




Ili kuweka mikono yako kuwa na muonekano mzuri wa asili na kuwa laini unatakiwa kuipa uangalizi wa kutosha ukiwa nyumbani. Mikono imekuwa ikitumika na kazi nyingi za nyumbani hata ofisini na wakati mwingine tumekuwa tukishika vitu ambavyo vinasababisha mikono kuwa migumu na hata iliyobabuka.
Watu wengi wamekuwa wakitengeneza nyuso zao na kusahau kabisa habari za kutunza mikono kitu ambacho si sawa sawa.
Unatakiwa kujifunza vitu gani vinatakiwa ili kuweza kuiweka mikono yako katika hali nzuri ikiwemo aina ya scrub na moisturizer ambayo itafanya mikono yako kuwa katika hali nzuri kila wakati.
Unaweza kutengeneza mikono yako ukiwa nyumbani  au hata saluni lakini kama utafanya mara moja kwa wiki utakuwa na mikono ambayo iinaonekana vizuri.
Ili kutengeneza mikono yako unatakiwa kuwa na nail file (tupa ya kucha), brashi ya mikono, kitu cha kukatia kucha (hata webe unafaa) losheni ya mikono, taulo sabuni na maji wa vuguvugu.
Unatakiwa kuosha mikono na ukate kucha na kisha anza kuzisugua taratibu kwa kutimua tupa.
Kisha weka maji ya vuguvugu kwenye beseni na tumbukiza mikono kaa kwa muda wa dakika tano ili kuwezesha ngozi ya mikono kulainika.
Kisha anza kusugua mikono taratibu unaweza kutumia kitambaa laini ila unachotakiwa kuhakikisha unasafisha hadi sehemu za katikati ya vidole baada ya hapo suuza mikono yako na ufute kwa taulo halafu paka lotion ya mikono. Njia nzuri pia ya kutunza mikono ni kuhakikisha unakula chakula chenye kulainisha mwili na kunywa maji mengi.
Kama unakuwa hujali mwili wako na hunywi maji mengi unaweza kuwa na mikono mikavu.

IFAHAMU SABUNI YA KURUDUSHA BIKRA.

Miongoni mwa maneno yaliyokwenye sabuni za kunawia ukeni.

 KUWA mrembo ni pamoja na kujikubali jinsi ulivyo na jinsi utakavyojiweka soap soapHata mtu akikupenda akupende  jinsi ulivyo. Pamoja na hayo kumekuwa na mambo mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya wanawake au wasichana kwa lengo la kufanikisha azma mbalimbali.
Miongoni mwa mambo hayo ni matumizi ya madawa mbalimbali ikiwemo yake ya kuongeza hips, makalio, kubadilisha rangi ya ngozi na hata kufanyia operesheni sura ili kuwa na muonekano ambao wanauona bora zaidi.
Pia kumekuwa na aina mbalimbali za sabuni kutoka ndani na nje ya nchi ambazo zimekuwa zikiuzwa ambazo zinadaiwa hurejesha ubikira zimesambaa sana madukani huku wateja wakubwa wakiwa ni wasichna na wanawake.

Hata hivyo walaatalam mbalimbali wanasema kuwa sabuni hhizo ambazo hutummika kwa kunawia sehemu za siti husaidia kurudisha bikira kwa mwanamke na hata kuwa na mnato.
Lakini wanaootumia sabuni hizo wameonywa kuwa  sabuni hizo zina kemikali zenye madhara makubwa kwa mtumiaji kwani zina uwezo mkubwa wa kusababisha kansa ya shingo ya kizazi.
Kwa mujibu wa Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka anasema hivi sasa kumekuwa na sabuni mbalimbali ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli.
Mtaalam huyo Anasema  Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji  yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano  kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa.
Pia michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi. Sabuni hizo zinatengeneza hali fulani ukeni  lakini haiwezi kurejesha hali ya maumbile iliyopotea.
Mfamasia huyo anasema wanaotumia sabuni hizo wako katika hatari kubwa ya kuambukuzwa magonjwa na hata kupata saratanni ya shingo a usazi kwani kemikali zinazotumika katika kutengeneza sabuni hizo zina athari kubwa kiafya.
Anataka wanawake kutatambua thamani yao na kuachana na matumizi ya sabuni hizo ambazo hazina manufaa yoyote na badala yake zimekuwa na madhara makubwa kwao.
Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Dodoma, Fredrick  Luyangi  anasema mrudiano wa athari hasa kwa matumizi ya sabuni huleta athari kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa taratibu bila mhusika kufahamu.Sabuni hizo husababisha kansa ya kizazi na kubainisha sabuni hizo licha kupigwa marufuku zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka ya vipodozi.
“Mara nyingi kwenye operesheni zinazofanyika zimekuwa zikiondolewa sokoni lakini hata hivyo zimekuwa zikiingizwa kwa wingi hali inayofanya zoezi la kudhibiti kuwa gumu” anasema.
Anawataka wanawake kuacha matumizi ya sabuni hizo ambazo zina madhara makubwa sana kwao kwani zikikosa wanunuzi zitaondoka sokoni.



USAFI KIPINDI CHA UJAUZITO.



Kipindi cha ujauzito wanawake wengi hujikuta wakiacha kuzingatia hatua mbalimbali za kujitunza ili kubaki warembo, matokeo yake hupoteza mvuto.

Hali hiyo inaweza kuendelea hata baada ya kujifungua na huenda ikawa mbaya zaidi kwa kuwa mara nyingi kipindi hicho mama hujikuta akitumia muda mwingi kumwangalia mtoto.

Kujifungua au ujauzito haiwezi kuwa sababu ya mwanamke kupoteza urembo uliokuwanao awali. Hivyo ni jukumu la mwanamke mjamzito au aliyejifungua kuhakikisha anabaki na mvuto wake ukiwa kwenye kiwango stahiki.

Kuwa mrembo siyo lazima upake vipodozi vyenye kemikali kwani vinaweza kumsababishia madhara mtoto kwa kuwa atatumia muda mrefu akiwa mwilini kwako.

Katika kipindi hiki mama mjamzito au aliyejifungua anatakiwa kuepuka kupaka mafuta, losheni au manukato yenye harufu kali inayoweza kuwa na madhara kwa mtoto hata kumsabishia wakati mgumu katika kupumua.

Ni vyema utumie vipodozi visivyo na kemikali ili kujilinda usipoteze mvuto wako. Pia tumia muda mwingi kufanya mazoezi mepesi yatakayoweza kukusadia kutengeneza umbile (shape), yako na kuifanya ionekane yenye mvuto wa hali ya juu hata ikiwa umetoka kujifungua.

Hakikisha pia kucha zako zinakuwa fupi na safi, hii haimaanishi kwamba huruhusiwi kupaka rangi unaweza kuziremba kwa mtindo wowote unaopenda lakini ziwe katika kiwango ambacho hakitamdhuru mtoto kwa namna yoyote.

Kitu muhimu cha kuzingatia katika kipindi hicho ni usafi na mwonekano wa ndani na nje. Kwa kufanya hivyo, hata mtoto atakuwa katika mazingira salama yanaweza kumtamanisha mtu mwingine kutaka kumshika.

NAMNA PAPAI NA ASALI INAVYOONDOA MADOA USONI.




Kuna maswali mengi yanayoulizwa jinsi ya kuondoa madoa usoni. Lakini jambo kubwa la kuangalia
je madoa uliyonayo
yamesababishwa na nini, Je ni kwa ajili ya kutumia madawa yenye kemikali kali kwa lengo la kupendezesha ngozi au ni
vipele tu vya kawaida.
Wengi wanapenda kutumia sabuni na cream kali ambazo baadaye zimekuwa zilileta madhara makubwa kwenye ngozi zao na
kuwafanya kuwa na mabaka meusi.
Ni muhimu pia kujifunza kutumia vipodozi vya asili ambavyo havina madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutumia mchanganyiko wa papai na asali kwa ajili ya kuondoa madoa usoni.
Mchanganyiko huu ambayo huwa laini utauacha ngozi yako ikiwa nyororo na yenye kuvutia.
Namna ya kutumia.
Kwanza ni kusafisha uso kwa maji ya vuguvugu kwa kutumia kitambaa laini  pia unaweza kusafisha hadi shingoni na hakikisha
uso umekataka kisha futa uso wako  na shingo kwa taulo.
Andaa asali yako pembeni kisha kata papai na kisha liponde hadi kulainika kabuisa.
Baada ya hapo changanya rojo hiyo ya papai na asali koroga hadi kuhakikisha umepata mchanganyiko mzuri.
Anza kupata usoni taratibu hadi maeneo ya shingo unaweza kukaa na mchanganyiko huo kwa robo saa kisha safisha uso
wako.
Unaweza kutumia mchanganyiko huu mara kadhaa kwa wiki mpaka upate matokeo mazuri kwenye ngozi yako.
Lakini jambo la msingi ni kuhakikisha anaepuka kutumia cream zenye kemikali kali kwani zimekuwa na madhara kwenye
ngozi.

ASALI KATIKA UREMBO WAKO



Mtaalam mmoja wa ngozi mwenye makazi yake mjini New York City ambaye pia ni daktari, Amy Wechsler anasema hali ya kunyunyurika iliyonayo asali na inayonasa inafanya kuwa kinga imara katika kidonda ambacho kinahitaji kisiingiliwe n vimelea na kutoa mazingira ya kuponya, hivyo asali ni bomba kwa tiba.

 Pamoja na tiba asali ni moisturize babu kubwa kwa ajili ya sura na mwili pia.
Asali ni dawa ya asili ambayo ina uwezo wa kukusanya maji  kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu a ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjo.

Mimi nakushauri jaribu moisturizing ya asali ambayo itaondoa ukavu wa ngozi yako na hata kuwasha na kutatarika.

Changanya vijiko vya mezani viwili vya asali na vijiko viwili vya mezani vya maziwa.
Kisha pasha moto mchanganyiko huo, kisha paka mchanganyiko huo katika uso wako na kupumzika kwa dakika kama kumi hivi.
Kisha jioshe kwa maji ya vuguvugu.Kama unataka kitu kama kosmetiki agiza lotion ya asali ili kuweka sawa ngozi yako.
Hakikisha unanunua lotion ambayo imetengenezwa kwa asali isiyochujwa.
Aina zote za asali zinasaidia kuondoa mikunjo ya uzeeni.

TUMIA ALOE VERA KUBORESHA MWILI


Kwa ukweli kuna mshindani mpya wa maji yanayorekebisha mwili wako na kuonekana mrembo zaidi. Watu wa urembo ambao walikazania unywaji wa maji ya dafu sasa wana kitu kipya mtaani, kinywaji cha aloe vera.

Aloe vera wataalamu wanasema kwamba ikinyweka katika maji inasaidia sana kuyeyusha chakula, kuondoa sumu zilizomo mwilini na kuondoa kiungulia lakini kubwa zaidi linabortesha muonekano wako.

Wataalamu wanasema pamoja na kuleta lishe katika mwili kuondoa tatizo la maji kwa ajili ya mwili na ngozi pia ina homoni mbili za Auxin na Gibberellins ambazo huleta kinga dhidi ya viungulia na pia kuleta uponyaji.

Kauliu hiyo imetolewa na mwasisi wa Sublime Beauty, Kathy Heshelow, Gibberellins zinaaminika kuchochea ukuaji wa seli mpya kwa kuimarisha fibroblasts amnbazo hutengeneza collagen.

Maji haya husafisha tishu za ngozi ambazo huathirika sana na sukari na pombe.

Mwili unapokuwa msafi na ngozi nayo inakuwa safi na  maji haya yanasaidia sana kuufanya mwili kuwa bora.

Maji ya aloe vera yanapatikana katika maduka makubwa lakini waweza tengeneza kwa namna hii:
chukua aunzi moja ya juisi changanya na aunzi nane za maji kila siku.

ONGEZA UREMBO WA NGOZI KWA KUTUMIA CHUMVI




Je, unafahamu kuwa chumvi inaweza kutumika kama scrub na kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia?
Matatizo ya chunusi, ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata ngozi iliyokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kuwafanya watumie vipodozi visivyo salama kwa ngozi zao.
Kwa kulitambua hilo, wataalamu wa urembo wa asili wamegundua kuwa chumvi ni scrub yenye gharama ndogo ambayo kila mtu anaweza kutumia tofauti na urembo mwingine wa ngozi.
Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi wanaolifahamu hili.
Unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii machoni mara utakapoanza kuitumia.

Mahitaji:
Chumvi ya unga kijiko kimoja kikubwa.
Jinsi ya kufanya:
Nawa uso wako kwa maji ya kawaida, chukua kitambaa laini na safi kisha chovya kwenye chumvi baada ya hapo sugua katika ngozi yako ya uso taratibu unaweza kuitumia hata mwilini.
Baada ya kupaka katika uso mzima, weka chini kitambaa chako kisha jisugue kwa kutumia mikono yako.
Fanya hivyo hadi utakapoona takataka za ngozi zinatoka kisha kaa kama dakika mbili.
Ukimaliza, osha kwa kutumia maji ya baridi.
Ni muhimu kufanya zoezi hili mara mbili kwa wiki kwani linasaidia kuondoa makunyanzi na kusafisha kabisa ngozi.

MAYAI YA KWARE SASA NI KIKOMBE CHA LOLIONDO


Hivi sasa kumeibuka tiba ya ‘mayai ya kwale’ ambayo inavuma kila kona na imekuwa gumzo kila mahali. Tiba hii ni ya kimaajabu kwani uvumi uliopo ni kwamba mayai ya kwale yana uwezo wa kutibu magonjwa yote sugu.
Kasi ya kushauri wagonjwa na hata wasio wagonjwa kutumia mayai haya badala ya kwenda hospitali kwa uchunguzi wa afya zao inaongezeka na maelekezo yanayopatikana mitaani juu ya kutumia tiba hii ni ya ajabu na yanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Nilishuhudia mtu mmoja akimwelekeza mgonjwa kuwa alipaswa kuyapasua mayai na kuyapondaponda pamoja na magamba yake na kisha ayanywe katika hali ya ubichi. Mwingine aliambiwa ayapasue na kisha ayakoroge pamoja na asali au maziwa kisha anywe, wengine wanaelekezwa kuyachemsha kama mayai ya kawaida na kisha kula kiini cha ndani. Uvumi huu unaenea kwa kasi mitaani.
Kutokana na kuvuma kwa tiba hii, mayai haya hivi sasa yanaonekana kusakwa kila mahali na yanauzwa kati ya Sh15,000 hadi 20,000 kwa trei.
Uvumi wa tiba hii hauna tofauti na ule uliozuka nchini juu tiba maarufu kama ‘kikombe cha Babu’. Watu wengi walikatisha matibabu kwenye hospitali mbalimbali na kuamua kwenda Kijiji cha Samunge kwenda kupata kikombe cha babu na kufanya kuwe na misururu mirefu ya watu waliokesha usiku na mchana. Hii ilizusha adha kubwa hasa kutokana na kutokuwepo na maandalizi ya vyoo hivyo watu kujisaidia ovyo vichakani.
Adha ya safari ndefu na kukaa kwenye foleni kwa zaidi ya siku tatu, kulifanya wenye afya mbaya kushindwa kuhimili na hata kupoteza maisha.
Katika mazingira haya ya kuibuka tiba za ajabuajabu ambazo hazijathibitishwa kitaalamu, ni vyema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikatoa ufafanuzi.
Isisubiri hadi watu wapoteze maisha halafu ndiyo ianze kuja na maelekezo tena yanayopingana na yale ambayo jamii inaamini. Kuchelewa kunafanya wengi wapoteze fedha na hata kuacha tiba sahihi na kukimbilia kitu ambacho kinavumishwa tu.
Serikali haipaswi kukaa kimya wakati watu wakiendelea kutibiana kwa vitu ambavyo havijathibitishwa kitaalamu.Kama Serikali ingechukua hatua mapema, watu wasingepoteza maisha kupitia kikombe cha babu.
Uvumi huu wa tiba ya mayai ya kwale hauna tofauti na Kikombe cha Babu.
Katika ulimwengu huu wa utandawazi na soko huria, ni kawaida kusikia mambo mapya yakiibuka kila kukicha, lakini kama mambo hayo yanagusa afya zetu, hatuna budi kuwa makini na waangalifu zaidi.

Umuhimu wa kukojoa baada ya tendo la ndoa.



Mara nyingi tunashauriwa kukojoa kila baada ya tendo la ndoa. Japokuwa wanawake wengi pamoja na kuwa na hamu ya kwenda haja ndogo kila baada ya tendo ila kutokana na uvivu na uchovu ujikuta katika usingizi mzito na kusahau tendo hili muhimu baada ya kufika kileleni. Umuhimu wa tendo hili ni kupunguza na kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa ya njia ya mkojo(U.T.I) na magonjwa ya zinaa(S.T.I)

Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa huongeza presha kwenye kibofu na kusababisha hamu ya kukojoa kila baada ya tendo hali inayokuwezesha kuondoa vimelea vya magonjwa mbali mbali kabla ya kusambaa kwenye kibofu na sehemu nyingine za mwili kusababisha matatizo makubwa. kwa wanaotumia kondomo pia unashauriwa kufanya hivo endapo itapasuka sambamba na kusafisha sehemu za uke na uume kwa maji safi na sabuni.
kwa wanaofanya mapenzi ya mdomo(chumvini na kulamba kone) unashauriwa kutoingiza shahawa, maji maji ya uke/ume na damu mdomoni kwani kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ukimwi na hepatitis B.

Umuhimu wa Limao katika Urembo wako.


Limao ni kitu kidogo sana lakini faida zake huwezi kuamini kama hujawahi kutumia. Kuna faida nyingi sana za kutumia limao, hasa wakati wa asubuhi wakati mwili umekaa bila kula usiku kucha. Kati ya nyingi, hizi hapa chache za kukufanya kufikiria kuanza kutumia limao kama utapenda.

Kusafisha mwili
Limao husaidia kusafisha uchafu usiohitajika mwilini kwa kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kulifanya ini kufanya kazi vizuri.
Kuweka harufu nzuri kinywani
Asidi iliyopo kwenye maji ya limao huua bakteria walioko mdomoni wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ni vizuri kama ukinywa limao baada ya kupiga mswaki ili kupata matokeo mazuri zaidi.
Kuleta nguvu mwilini
Limao baada ya kuingia kwenye mfumo wa chakula, huupa mwili nguvu. Hii husaidia kuondoa uchovu na msongo wa mawazo, sonono (depression), na wasiwasi.
Kupunguza uzito
Nyuzinyuzi za pectin (Pectin fiber) zilizomo kwenye limao husaidia kuzuia njaa na hivyo kutopata hamu ya kula mara kwa mara.
Kuongeza kinga ya mwili
Malimao yana acid, ni chanzo kizuri cha vitamin C, ambayo ni nzuri kuzuia baridi na homa. Malimao pia husaidia kuimarisha ubongo na mishipa ya fahamu kutokana na kuwa na madini ya Potassium. Vilevile Potassium husaidia kuzuia shinikizo la damu.
Kuzuia uvimbe
Cha kushangaza kabisa, ukiwa unakunywa maji ya limao mara kwa mara, unapunguza kiwango cha acid mwilini mwako. Hii ni kutokana na ukweli kuwa limao haitengenezi acid mwilini baada ya kumeng’enywa. Kutokana na hii, husaidia sana kupunguza asidi ya uric ambayo ni chanzo kikuu cha uvimbe mwilini.
Kuondoa mikunjo na makovu mwilini
Maji ya limao huweza kuondoka makovu na mikunjo kwenye ngozi. Huweza vilevile kupunguza makovu makubwa kama ukinyunyizia kila mara. Kutokana na uwezo wake wa kusafisha damu, maji ya limao huacha ngozi ikiwa inang’aa na yenye afya.
Husaidia kukufanya uache kunywa kahawa
Je wewe ni mlevi wa kahawa na unataka njia ya kuacha ? Basi kunywa kikombe cha maji ya moto chenye mchanganyiko wa limao. Hii ni dawa tosha. Huwezi kuamini hadi ujaribu, na ukishajaribu hutoweza kurudi tena kwenye kahawa.
Je unatakiwa kutumia limao kwa kiwango gani?
Kama una uzito mdogo, chini ya kilo 70, unaweza kula nusu limao, kama umezidi kilo 70 unatakiwa kula limao zima kwa siku. Ukifanya hivi kila siku utaanza kuona mabadiliko muda si mrefu.

UZURI WA MAYAI NA NYAMA YA KWARE KATIKA KUKUKINGA NA MARADHI MBALIMBALI.


Katika siku za hivi karibuni ndege aitwae kware ameanza kuwa ndege maarufu katika baadhi ya wafugaji katika nchi yetu na kwa wale ambao walikuwa wakiwawinda porini enzi hizo bado wana imani kuwa ndege huyu hawezi kufungwa kama hatakimbia basi atajiua, lakini kwa wale wanaotaka kumfuga ndege huyu mdogo mwenye mayai matamu ya madoa doa wanaweza sasa inaweza kugeuka chanzo cha mapato na sehemu ya chakula bora kwa familia.
Leo ningependa niingie ndani kuwa nini hasa tofauti ya mayai ya kware na yale ya kuku ingawa taarifa nyingi nilizopata kwenye mitandao na kwinginekoinaonyesha tu kwa habari za watu waliopata kutumia mayai kware na kuona umuhimu wake katika afya na baadhi ya tovuti kuongelea tu kwamba mayai haya ni mazuri yanasaidia kwa afya bado kama watu wanaotaka kueleew inakuwa haikidhi haja kuamani tu yakuwa yana saidia katika afya, nikiwa mmojawapo wa watu ambao niliona yanasaidia watu walikuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakiendelea vizuri.
 

Na mpaka sasa mimi napenda kukiita hiki chakula bora na sio dawa kama watu wengi waliotumia wakapata nafuu kwa yale waliokuwa yakiwasibu na wale waliokuwa na dhaifu nyingine katika mwili wakarejea afya maridhawa lakini msimano wangu binafsi napenda kutambua mchango wa haya mayai kama chakula bora.

Ndio maana hata Mungu aliamua kuwapa wana waisrael kama chakula kwenye Kutoka 16:13 na mtumishi Daudi anakomelezea kwenye Zaburi 105:40. Sasa kwa kuwa siku zote najua kuwa Mungu hapingani na sayansi kitu wanasayansi wanachofanya nikungudua tu mambo ambayo Mungu ameyaweka kwahiyo ikabidi nitafute kisayansi sasa sisi tunaopenda kuoona na kufanya akili zetu zielewe maana ukielewa jambo kwenye akili yako ni rahisi kufanyia kazi.
 

Katika kutafuta nikasema pamoja na vyanzo vya wataalamu binafsi ningependa kupata vyanzo vilivyo vya kiserekali ambavyo wao hawana upande waliolalia maana hawa wataalamu binafsi wanaweza kuwa na ajenda zao, Na ndipo nilipopata utafiti wa USDA (United State Department of Agriculture) unaonyesha tofauti za mayai haya kwa kina katika category 78 za nutrients zilizogawanya mayai ya kware yana vitu 31 zaidi ambayo ya kuku hayana kabisa wakati yale ya kuku ya kitu kimoja tu ambacho hakiko kwenye ya kware ambacho naomba nikitaje nacho ni Vitamin K (phylloquinone) na katika hizo 45 vilivyobaki vya kware 42 viko juu na vingine hata mara mbili ya zile za kuku, wakati vya kuku ni 3 vitatu ambayo vimezidi vile vya kware.

Faida hizi zote tunaweza kupata kama watu wetu watajiingiza katika ufugaji wa ndege huyu ambaye anapatikana sehemu nyingi unaweza kuanza kidogo kidogo mpaka wakafikia mwengi,na kama unavyooana hapo juu unaweza kutengeneza banda rahisi la mbao laini na wafu na kuanzia hapo, ila wawapo wadogo waweke kwenye box na kuwawekea taa kama ufanyavyo kuku.
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency