Home » » Utunzaji wa Uso

Utunzaji wa Uso

 
                           Watu wengi wamekuwa wakichukulia suala la utunzaji wa ngozi ya uso kwa umakini zaidi. Ngozi zina mahitaji maalum ikiwemo kuweka ngozi katika hali ya usafi na pia kuikinga ngozi na miale ya jua na mabadiliko mengine ya hali ya hewa. Ngozi ya uso inahitaji umakini zaidi kwani uso ni utambulisho wa jinsi ulivyo na imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi kwa sababu uso umekuwa ukizalisha mafuta mengi hasa kwenye paji la uso, macho, pua, na kidevu. Hitaji muhimu ni kuhakikisha kuwa, ngozi yako inakuwa katika hali nzuri na safi kuanzia asubuhi unapoamka hadi usiku unapokwenda kulala. Unatakiwa kuchukua dakika tano hadi 10 katika suala hili.
                          Utunzaji wa uso asubuhi Wakati wa asubuhi unatakiwa kusafisha uso wako kwa maji ya vuguvugu. Epuka kutumia sabuni ya mche (ya kufulia) kwani haikutengenezwa maalum kwa ajili ya uso na imekuwa ikifanya ngozi ya uso kuwa iliyokakamaa Unatakiwa kuhakikisha kuwa, uynaosha uso wako vizuri wakati unaoga au wakati unanawa uso kwenye sinki, Unaweza kutumia tona kusafisha uso wako kwani husaidia kuondoa uchafu ulioganda usoni. Baadaye unaweza kutumia moisturiza . Utunzaji wa uso jioni Jioni unaweza kusafisha uso wako kwa kutumia maji ya vuguvugu. Baada ya mizunguko ya hapa na pale ngozi inakuwa imechoka na inahitaji umakini zaidi katika suala la usafi. Pia unapotumia tona jaribu kutumi pamba laini ili kuweza kulinda uso wako. Unapotunza ngozi lengo ni ngozi kuwa na unyevunyevu, unatakiwa kuhakikisha haina magamba. Lakini pia unaweza kutoa magamba au ngozi iliyokufa ambayo hufanya ngozi isiyokubalika.
                          Wakati mwingine ngozi isiyokubalka husababuisha uso kuwa na chunusi. Angalizo Usiende kulala bila kuondoa make -up usoni. Make-up zimekuwa zikisababisha kuzina kwa vitundu vya kutolea hewa na hivyo kusababisha tatizo la kuwa na ngozi isiyokubalika. Pia unatakiwa kuacha kutumia vipodozi vyenye kemikali kwani hufanya watu wengine kupata kansa za ngozi.Wakati mwingine sehemu za uso hupata uvimbe . Hizi ni moja ya changamoto zinazoweza kukutokea katika ngozi yako la muhimu ni kuhakikisha kuwa, usafi unazingatiwa sana pamoja na kunywa maji mengi, mboga za majani na matunda kwa wingi.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency