Home » » Uvaaji wa Soksi

Uvaaji wa Soksi


                  Soksi ni vazi ambalo huvaliwa miguuni. Miguu ni mmoja kati ya viungo ambavyo vinatoa jasho mwilini, huzalisha zaidi jasho kila siku. Soksi husaidia kuhakikisha kuwa unyevunyevu unahifadhiwa katika eneo linalotakiwa na baadaye kutolewa nje kwa njia ya hewa. Katika mazingira ya baridi soksi husaidia kupunguza uhakika wa kupata baridi. Soksi hutengenezwa kwa pamba, sufu, nailon na aina nyingine za nyuzi. Katika kuongeza kiasi cha ulaini, malighafi nyingine ambazo hutengenezaa soksi hutumika. Kuna aina mbalimbali za rangi za soksi ambazo hutengenezwa na pia kuvaliwa kila siku.
                     Wengine huvaa soksi ili kuimarisha muonekano wao Soksi za rangi ya kung’aa mara nyingi huwa ni sehemu ya vazi katika michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutofautisha wachezaji pale ambapo miguu pekee ndiyo inaonekana. Mitindo ya soksi huvaliwa kulingana na matakwa ya mvaaji. Wengine hupenda kuvaa soksi na viatu vya wazi huku wengine wakivaa na viatu vilivyozibwa. Soksi ndefu nyeupe huvaliwa kama sehemu ya sare za shule.
                     Wanamichezo wamekuwa wakitumia soksi kama sehemu ya vazi. Soksi hizi huwa ndefu na mara nyingi huwa ni nzito. Makundi mbalimbali yamekuwa yakivaa soksi hata wanawake ambao huvaa soksi katika kuhakikisha wanakuwa na muonekano mzuri na mavazi waliyovaa. Kuna zile soksi nyepesi sana hizi mara nyingi huvaliwa na wanawake. Soksi ni vazi ambalo huvaliwa kila siku hasa kwa wanaume ni vizuri kama soksi zinakuwa safi muda wote ili kuondoa ile harufu mbaya ambayo imekuwa kero kwa watu wengi. Ni vizuri kama soksi zikafuliwa na kuanikwa juani na kukauka vizuri kabla ya kuvaliwa.
                         Pia wavaaji wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na jozi nyingi za soksi ili kuweza kupunguza ugumu wa kuzitunza.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency