Home » » Part 3:Huu ndio ushaidi wa kesi ya mbasha

Part 3:Huu ndio ushaidi wa kesi ya mbasha



Ushahidi wa kesi inayomkabili mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha utaanza kusikilizwa Agosti 22, mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya Ilala.

Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, anakabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji.

Mahakama imepanga tarehe hiyo kuanza kusikiliza ushahidi na upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne.

Jana mshtakiwa huyo alisomewa maelezo ya awali na Mbasha alikana baadhi ya maelezo na kuyakubali mengine.

Akisoma maelezo hayo, wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai kuwa Mei 23 mwaka huu katika nyumba ya mshtakiwa iliyopo Tabata Kimanga, mshtakiwa alimuingilia kimwili msichana wa miaka 17, walipobaki wawili katika nyumba hiyo.

Wakili Katuga alidai siku hiyo ya tukio mshtakiwa alifanikiwa kufanya mapenzi na binti huyo na kumwambia asimwambie mtu wakati mkewe akiwa hayupo nyumbani hapo.

Aliendelea kudai kuwa Mei 25, mshtakiwa alimwambia binti huyo amsindikize kwenda kumtafuta Flora sehemu alipo na wakati wanarudi kutoka huko, mshtakiwa alifanya mapenzi na binti huyo ndani ya gari lake alilokuwa akiendesha mshtakiwa.

Katuga alidai Mei 26, mwaka huu, binti huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Osterbay akapewa PF3 na kwenda Hospitali ya Amana kutibiwa na vipimo vya daktari vilithibitisha kuingiliwa kimwili.

Wakili Katuga alidai baada ya binti huyo kutoa taarifa polisi, Mbasha alitoweka nyumbani hadi Juni 16, mwaka huu, alipofikishwa polisi na Juni 17 alipandishwa mahakamani hapo kujibu mashtaka mawili ya kubaka.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency