Home » » Tambua ugonjwa wa Ebola na namna ya kujikinga

Tambua ugonjwa wa Ebola na namna ya kujikinga

Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na kirusi kiitwacho ebola. Kirusi hicho ni moja kati ya familia ya virusi watatu toka katika familia ya filoviridiae.
Zipo aina tano za kirusi cha ebola ambao nao ni bundibugyo ebolavirus (BDBV), zaire ebolavirus (EBOV), reston ebolavirus (RESTV), sudan ebolavirus (SUDV) na tai forest ebolavirus (TAFV).
Aina hizo tatu za virusi, yaani BDBV, EBOV na RESTV, ndiyo inayongoza kwa kusababisha mlipuko wa ugonjwa huo barani Afrika. Wengine wanapatikana nchi za Asia, yaani Ufilipino na Thailand na mpaka sasa hakuna taarifa za kusababisha vifo.
Kwa mara ya kwanza ugonjwa huu uliripotiwa kutokea mwaka 1976 katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hatari ya mgojwa kupoteza maisha ni asilimia 90. Watu ambao wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo ni jamii inayoishi karibu na jamii ya wanyama au watu walioathirika.
Pia uwepo katika mazishi ya wagonjwa wa ebola wakati wa shughuli za kuzika na kugusana na majimaji ya mgonjwa aliyekufa.
Unavyoambukizwa na kuenea
Chanzo cha ugonjwa katika makundi yetu ni mtu mmojawapo kugusana na damu au majimaji ya wanyama waliombukizwa, ambao mara nyingi ni nyani, sokwe, tumbili na popo. Inaaminika kuwa popo wanaopenda kula matunda, wanaeneza ugonjwa huo bila wao kuaathirika.
Katika jamii yetu ugonjwa huu huweza kuambukizwa kutoka mtu mmoja mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine baada ya kugusana na damu au maji maji kupitia michubuko au majeraha juu ya ngozi.Watu walio na maambukizi na wakapata nafuu bado wanaweza kuwaambukiza wengine kwa zaidi ya miezi miwili, pia wanaweza kuwambukiza watu wengine kwa njia ya kujamiana.
Dalili za ugonjwa
Jina jingine la ugonjwa huu ni ‘ugonjwa wa kuvuja damu’. Hii ilitokana kujitokeza dalili ya kuvuja damu mwilini.Dalili za ugonjwa huu huu huanza kujitokeza kuanzia wiki ya pili au ya tatu tangu kugusana na damu au majimaji ya mwilini ya mgonjwa wa ebola.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency