Home » » Umuhimu wa Limao katika Urembo wako.

Umuhimu wa Limao katika Urembo wako.


Limao ni kitu kidogo sana lakini faida zake huwezi kuamini kama hujawahi kutumia. Kuna faida nyingi sana za kutumia limao, hasa wakati wa asubuhi wakati mwili umekaa bila kula usiku kucha. Kati ya nyingi, hizi hapa chache za kukufanya kufikiria kuanza kutumia limao kama utapenda.

Kusafisha mwili
Limao husaidia kusafisha uchafu usiohitajika mwilini kwa kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kulifanya ini kufanya kazi vizuri.
Kuweka harufu nzuri kinywani
Asidi iliyopo kwenye maji ya limao huua bakteria walioko mdomoni wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ni vizuri kama ukinywa limao baada ya kupiga mswaki ili kupata matokeo mazuri zaidi.
Kuleta nguvu mwilini
Limao baada ya kuingia kwenye mfumo wa chakula, huupa mwili nguvu. Hii husaidia kuondoa uchovu na msongo wa mawazo, sonono (depression), na wasiwasi.
Kupunguza uzito
Nyuzinyuzi za pectin (Pectin fiber) zilizomo kwenye limao husaidia kuzuia njaa na hivyo kutopata hamu ya kula mara kwa mara.
Kuongeza kinga ya mwili
Malimao yana acid, ni chanzo kizuri cha vitamin C, ambayo ni nzuri kuzuia baridi na homa. Malimao pia husaidia kuimarisha ubongo na mishipa ya fahamu kutokana na kuwa na madini ya Potassium. Vilevile Potassium husaidia kuzuia shinikizo la damu.
Kuzuia uvimbe
Cha kushangaza kabisa, ukiwa unakunywa maji ya limao mara kwa mara, unapunguza kiwango cha acid mwilini mwako. Hii ni kutokana na ukweli kuwa limao haitengenezi acid mwilini baada ya kumeng’enywa. Kutokana na hii, husaidia sana kupunguza asidi ya uric ambayo ni chanzo kikuu cha uvimbe mwilini.
Kuondoa mikunjo na makovu mwilini
Maji ya limao huweza kuondoka makovu na mikunjo kwenye ngozi. Huweza vilevile kupunguza makovu makubwa kama ukinyunyizia kila mara. Kutokana na uwezo wake wa kusafisha damu, maji ya limao huacha ngozi ikiwa inang’aa na yenye afya.
Husaidia kukufanya uache kunywa kahawa
Je wewe ni mlevi wa kahawa na unataka njia ya kuacha ? Basi kunywa kikombe cha maji ya moto chenye mchanganyiko wa limao. Hii ni dawa tosha. Huwezi kuamini hadi ujaribu, na ukishajaribu hutoweza kurudi tena kwenye kahawa.
Je unatakiwa kutumia limao kwa kiwango gani?
Kama una uzito mdogo, chini ya kilo 70, unaweza kula nusu limao, kama umezidi kilo 70 unatakiwa kula limao zima kwa siku. Ukifanya hivi kila siku utaanza kuona mabadiliko muda si mrefu.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency