Home » , » MAVAZI YANAVYOATHIRI MUONEKANO WA MTU.

MAVAZI YANAVYOATHIRI MUONEKANO WA MTU.




Muhimu kutambua mavazi ni njia kubwa na nzuri ya kutambulisha tabia ya Mtu. Wengi wanapendwa au wanachukiwa kutokana na mavazi wanayovaa. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na heshima ama kwa kuwa mafupi au yamekuwa yakiacha sehemu kubwa ya kifua kuwa wazi.
Wasichana wa sasa wanaona kuvaa nguo zinazoacha wazi sehemu kubwa ya matiti kama fasheni.
Kuna mavazi ya aina nyingi ambapo yakivaliwa humfanya mtu apendeze au achukize. Uvaaji wa nguo unatakiwa kuzingatia umri na rangi ya mwili na pia mazingira ya nguo inapovaliwa.
Sio kila nguo ni ya kuvaliwa mchana na sio kila nguo ni ya kutoka nayo barabarani aina nyingine za nguo hazistahili kuvaliwa barabarani unapotoka tu barabarani unaanza kupigiwa miluzi hiyo si sawa sawa.
Mathalani wewe ni mfanyakazi unajua unatakiwa uvaaje, kujiweka mrembo na mtanashati ni kitu muhimu. Siku hizi kuna mitimbo mbalimbali ya nguo za madukani, kushona mitindo ya kutumia vitenge, vitambaa kwa mitindo ambayo inatunza heshima ya mvaaji.
Unatakiwa kuvaa kulingana na mahali na wakati kwani kuna nguo za kazini na za kutokea lakini sasa hivi si ajabu ukakutana na mtu mchana wa jua kali akiwa amevaa nguo ya usiku au kumkuta akiwa amevaa viatu virefu huku akijua fika anatembea kwa miguu kwa umbali mrefu.
Share this article :
 
Copyright © March 2012. MARIDADI AGENCY
-Haki zote zimehifadhiwa
- All Rights Reserved
Template Modified by Hassan Moh Toziri
Published by Maridadi Agency