Wakazi wa eneo la Sakina wamefanikiwa jijini Arusha wamefanikiwa kumuua chatu mkubwa aliyesadikia ni wa kimazingara .
Aidha jambo la kushangaza zaidi mama ambaye chatu huyo aliyekuwa akitoka ndani ya makazi yake alionekana akishikwa kadhabu na kugombana na waliofanikisha zoezi kwa madai ya kutotaka chatu huyo adhuliwe.
Baada ya kuonekana kwa chatu huyo akiranda huku amefungwa kitambaa chenye maandishi ya kiarabu yasiyoeleweka vizuri,wananchi walijipanga kuweza kumuangamiza chatu huyo.
Baada ya kupambana kwa muda mfupi walifanikiwa kumkata kata chatu huyo kwa ujasili mkubwa.
Wakazi wengi wemehusisha tukio hili na imani za kishirikina zinazoendelea kutawala mioyo ya watu wengi dhaifu wanaotaka mafanikiwa kwa haraka na njia rahisi zaidi.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO