Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja ambaye hakujulikana jina lake wala kujua anapoishi, anasadikika kutenda ukatili na unyama wa hali juu kwa kumuua huyo mwanaye na kisha kumtupa pembezoni mwa barabarani
Mtoto mchanga (pichani juu) ameokotwa kandokando ya barabara ya Kawe-Beach, huku puani na mdomoni akiwa amefungwa plasta kabla ya kutupwa kwake, iliyosababisha kukosa pumzi na kufariki.
Wavuvi wa eneo hilo waliona mfuko pembezoni ukiwa na damu hali ambayo iliwashtua na kuamua kusogea karibu, ndipo walipomkuta mtoto huyo mwenye jinsi ya kike, akiwa amefariki huku akiwa amefungwa plasta mdomoni na puani.
Aidha inasemekana motto huyo alifungwa blasta mdomoni ili tu kuzuia sauti ya kilio ambacho kingeweza kuwastua wakazi wa jirani na plast iliyokuwa puani ni kuhakikisha mauti inamfika kabla ya kuokotwa na mtu yoyote.
Tunaendelea kulani matukio ya kunyama yanayoendelea kufanyika na jeshi la polisi linaombwa kwa mkazi yoyote ambae anahisi anamtambua muhusika wa kitendo hichi basi amfike kituo chchote cha polisi cha jirani ili sharia ichukue hatua zake dhidi ya ukatili huu.
0 comments:
BONYEZA HAPA KUACHA MAONI YAKO